Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson amezindua Taasisi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kama Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF) ambayo ina lengo la kusaidia jamii katika masuala ya afya, elimu na uchumi.

 Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Sapanjo Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

Dr. Tulia amewapongeza Wanawake wa Chunya kwa kumuunga mkono Mhandisi Maryprisca Mahundi, ambapo amesema>>> "Naungana naye kuwashukuru wanawake kwa kumchagua Mahundi kuwawakilisha nakuomba uendelee hivyo hivyo"

Aidha Dr. Tulia amempongeza Eng. Mahundi kwa kuwawezesha Wanawake kiuchumi kwa kuwaanzishia miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa makalasha lakini zaidi kwa kuwawezesha Wanawake wa Chunya shilingi milioni kumi na moja kwa ajili ya kuanzisha mradi wa kiuchumi.