Sept 27, 2021: "Meneja wa RUWASA mkoa, hili lipo ndani ya
uwezo wako. Nakupa wiki mbili hili tatizo liwe limemalizika. Taarifa inaeleza
kuwa kuna upungufu wa maji, halafu hayo yanayopatikana kidogo bado yanavuja.
Hili tatizo limalizike haraka."
Ni kauli ya Naibu Waziri wa Maji Mhandishi Maryprisca Mahundi
wakati akimpa maagizo Meneja Wakala wa Maji RUWASA Mkoani Njombe Sadick Chaka baada
kushuhudia uvujaji wa maji kwenye Tenki la kijiji cha Usulilo wilayani Makete
mkoani Njombe.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ametoa wiki mbili kwa Meneja wa Maji Mkoa wa Njombe (RUWASA) Mhandisi Sadick Chakka kuhakikisha tatizo la uvujaji wa maji katika tenki hilo linapatiwa ufumbuzi.
Mhandisi Maryprisca alikagua na kubauni kuwa tanki hilo linavuja hali ambayo
inasababisha kupungua kiwango cha maji yanayokusudiwa kuwafikia wananchi.
Naibu Waziri. Mhe. Mahundi yuko ziara ya kikazi mkoani Njombe
kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maji.
0 Comments
Post a Comment