Naibu Waziri wa Maji
Mhandisi Maryprisca Mahundi ameshiriki kwenye hafla maalumu ya kukabidhiwa
mitaji kiasi cha zaidi ya Sh Mil 200 kwa vikundi 10 vya wajasiriamali wa
Halmashauri ya wilaya ya Mbeya na kuwataka kuelekeza mikopo waliyopata kwenye
mitaji.
Mhandisi Maryprisca
amesema Mheshimiwa Rais Mama Samia anapenda kuona wananchi wanapata unafuu wa maisha kwa kupatiwa mitaji
ili iwainue kiuchumi.
Amewataka wanufaika
wa mikopo hiyo kuielekeza kwenye malengo waliyokusudia ili kuweza kurejesha kwa
urahisi ili kufungua wigo kwa wengine kupata mikopo.
‘’Hakikisheni mikopo
mliyopewa isiwagawanye,kopa kwa busara lipa kwa wakati mkopo mliopewa
ukawaunganishe na kuwapa mafanikio baada ya kuzalisha faida’’amesema Mhandisi
Maryprisca.
Amebainisha kuwa
mikopo hii isiyo na riba ni matunda ya Rais Samia Suluhu Hassan ambayo
itaenda kuimarisha uchumi na kubadilisha
mifumo ya maisha yao ikiwa ni pamoja na kupata elimu ya namna bora ya kutumia
mikopo hiyo.
Aidha Mhandisi
Maryprisca ametumia fursa hiyo kuelezea namna ambavyo Wizara ya Maji
inavyoendelea kuimarisha mifumo ya maji kwa kukarabati miundo mbinu chakavu ili
huduma ya maji isogezwe karibu na makazi ya watu.
‘’
0 Comments
Post a Comment