*BEI KUBWA VIFURUSHI VYA DATA MWIBA MAENDELEO YA KIDIGITALI TANZANIA*




-Wadau walia kila kona ya nchi


-Tasnia ya habari za kidigitali, elimu, Dini,    Burudani vyatajwa kuathirika 



Dar es salaam, 

Kutokana na kupanda maradufu kwa bei za vifurishi vya interneti nchi huku GB 1 ya Data ikipatikana kwa zaidi ya dola 1.3 kumesababisha kupungua kwa kasi idadi ya watumiaji wa internet nchini hivyo kuathiri taasisi, mashirika na watumiaji binafsi wa interneti ambao hutumia huduma hiyo katika majukumu mbalimbali pamoja na burudani.


Aidha, kutokana na bei hizo kutokuwa rafiki kwa watumiaji wa huduma hiyo hasa mwananchi wa kawaida Taasisi na tasnia mbalimbali zimetajwa kuathirika kwa namna moja au nyingine


-Tasnia ya habari za kidigitali. Watoa huduma za maudhui katika Tovuti na programu tumishi na mtandao wa YouTube wamelalamika kutokana na kushuka kwa kasi kwa watumiaji wa huduma zao huku wakiiomba wizara na wadau husika kujadili na kulipatia mwarobaini suala hili 


-Tasnia ya burudani,

Wasanii na watoaji maudhui  ya burudani hasa kwa mtandao wa video wa YouTube nao wamedai idadi ya wanaofuatilia kazi zao kushuka kwa kasi kwa siku za karibuni, jambo ambalo wamedai kuathiri sana kipato chao. Vilevile mitandao mbalimbali ya takwimu inaonesha kushuka kwa watumiaji wa mtandao wa YouTube Tanzania kwa siku za karibuni.


-Watumiaji binafsi,

Watumiaji mbalimbali wa internet Tanzania nao wameonesha kukerwa na kupanda Mara kwa Mara kwa bei za vifurushi huku wakidai uishaji wa haraka kuliko kawaida wa vifurushi hivyo, vile vile hawakuacha kukumbusha ahadi za wadau na wizara kuahidi mara kadhaa kulishughulikia tatizo hilo na kubakia ahadi hewa. 



Pamoja na hayo, Bei hizi ambazo zimetajwa kutokuwa rafiki kwa watumiaji  huenda zikazidi kuathiri  mfumo mzima wa maendeleo ya kidigitali hasa kwa mashirika, taasisi, na makampuni kama vile huduma za kibenki za kidigitali, huduma za afya, elimu, na dini zinazopatikana kwa njia za kidigitali pamoja na tasnia ya michezo ya bahati nasibu ya mtandaoni. 


Wadau Watoa ushauri, 

Wadau mbalimbali wanaishauri  wizara husika, pamoja na makampuni yanayotoa huduma hiyo muhimu kwa maendeleo kuangalia upya na kwa umakini jambo hili kwa maendeleo na tija ya nchi.