DR TULIA APEWA SAPOTI NA NMB BATI ZA MABWENI WATOTO WA KIKE CBE KAMPASI YA MBEYA


Na Rashid Mkwinda, Mbeya Yetu Tv

NOV.6,2021:MBUNGE wa Jimbo la Mbeya Dr Tulia Ackson amekabidhi bati 500 zenye thamani ya Shilingi Mil 12 kwa ajili ya ujenzi wa Mabweni ya Watoto wa kike kwa Chuo cha Biashara CBE Kampasi ya Mbeya.

Bati hizo ambayo ni sapoti kutoka Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu zimetolewa ili kusaidia kupunguza adha kwa watoto wa kike kukaa mbali na mazingirachuo.

Akizungumza wakati akikabidhi bati hizo kwa Uongozi wa chuo cha Elimu ya Biashara CBE Jijini Mbeya Dkt Tulia ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na mlezi wa Chuo hicho amesema  anatumia fursa hiyo kuwashukuru Benki ya NMB kwa msaada huo na kuzitaka taasisi zingine ziige mfano wa Benki ya NMB.

Amesema kuwa sapoti hiyo itaongeza ari na hamasa kwa watoto wa kike kusoma kwa bidii huku wakiishi katika mazingira rafiki ya chuo badala ya kupanga jambo ambalo litawapunguzia vishawishi nje ya masomo yao.

‘’Msaada huu ni mkubwa utakamilisha kukamilisha kuezeka hosteli zote,tunawaomba wadau walioahidi waendelee kutoa msaada tunapokea kitu chochote kinachohusu ujenzi’’

Dr Tulia amesisitiza  wadau waendelee kuchangia kutokana umuhimu wake kwa Watoto wa kike hususan kutokana na mtazamo tofauti kwa kupigiwa mfano Rais aliyeko madarakani ambaye ni mwanamke na kuwa mtoto wa kike akiendelea kulindwa anaweza kuwa kiongozi mkubwa.

‘’Nimelipa umuhimu mkubwa tukio hili kwa kuja mwenyewe huku Bunge likiendelea mjini Dodoma,mimi ni mlezi wa Chuo hiki,tuendeleze juhudi hizi yeyote mwenye mchango wake nitamfuata aliko ili aendelee kutusapoti kwenye jambo hili’’

Awali Meneja wa NMB Kanda Nyanda za Juu Straton Chilongola amesema Benki hiyo imeshiriki kuchangia ikiwa ni sehemu ya mchango unaotokana na faida yake kuchangia  huduma za kijamii kwenye sekta ya elimu.

Naye Mkurugenzi wa CBE Kampasi ya Mbeya Tumaini Jeremiah amemshukuru Dkt Tulia kutokana na ushawishi na hamasa yake kubwa ambayo imesababisha Benki ya NMB kutoa sapoti hiyo ambapo amezitaka taasisi zingine kuiga mfano wa NMB.