BENKI ya NMB Plc imekanusha taarifa za uvumi zilizozagaa mitandaoni kwamba inaendesha shindano litakalomfanya mteja ajinyakulie kitita cha Sh. 500,000/-.


Taarifa hizo zinamtaka mteja kujibu Swali ambalo limeulizwa kwa lugha ya Kiingereza Do You Know NMB Bank Plc? ambapo mteja ametakiwa kujibu YES au NO.


Kufuatia taarifa hizo Benki ya NMB, Novemba 17,2021 imetoa ufafanuzi mtandaoni na kueleza kuwa taarifa hizo si sahihi kwa kutoa tahadhari kwa wateja.


"Hatuendeshi shindano lolote la namna hii,Epuka Kushiriki kwani ni utapeli"


Taarifa hiyo imeongeza kwa kuandika maandishi yaliyokolezwa(Bolded) kwa rangi nyekundu [FAKE].