Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam
Taasisi ya Vyombo vya Habari Tanzania(Tanzania Media Foundation -TMF) imekutana na Waandishi wa Habari za Mitandao nchini na kuwataka kuwa na msingi wa awali wa uandishi kwa kuandika habari za ukweli.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TMF Dastan Kamanzi amesema kuwa uandaaji wa habari unapaswa kuzingatia ukweli na ubobezi kwa kile ambacho Mwandishi wa Habari anataka kuwapatia wasomaji wake.
‘’ Msingi wa uandishi wa Habari ni ukweli hivyo ni muhimu Waandishi wa Habari kuzingatia msingi huo. kila wanapoandaa habari’’amesema Kamanzi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Nukta Africa Nuzulack Dausen amesema asilimia kubwa ya waandishi wa mitandaoni hawazingatii mizani na ukweli kwa habari wanazoandika na hivyo kuacha mambo muhimu yanayoweza kuisaidia jamii katika habari zao.
Dausen amebainisha kuwa changamoto inayosababisha hali hiyo ni ni pamoja na habari hizo kutoacha athari au kuleta mabadiliko chanya katika jamii huku kukiwa na taarifa zenye vichwa vya habari ambavyo havifanani wala kuendana nahabari husika.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Asha Shaban na Joseph Mwaisango wameelezea umuhimu wa mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na kuendelea kuandika habari za ukweli sanjari na kuboresha uandishi kwa kuhakiki taarifa zao kabla ya kuchapishwa.
Mafunzo
ya hayo ya Uhakiki wa Habari yameandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari
Tanzania (Tanzania Media Foundation -TMF) ambayo yanafanyika kwenye ofisi za TMF
Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kuwajumuisha Waandishi wa Habari za Mtandao
kutoka mikoa ya Shinyanga, Tabora, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mara, Mbeya na
Iringa.
0 Comments
Post a Comment