BILIONEA MZEE MAJINJAH ABISHIWA HODI
NYUMBANI KWAKE
Binti yake Avikwa Pete ya Uchumba
Jumapili ya Oktoba 31,2021 ililikuwa ni
siku iliyojaa hoihoi vifijo na nderemo ambayo imejenga historia kubwa kwa
maisha ya Binti wa Bilionea na mwekezaji mkubwa nchini, Mzee Majinjah,Tunsubilege
Kabungo.
Mzee Majinjah na Mama Majinjah hawakusita kuonesha bashasha na furaha ya wazi kwa namna ambavyo Binti yao amewapa heshima kubwa wazazi wake waliyemzaa,kumlea na kumsomesha.
Mzee Majinjah anasema jambo hili ni
la kipekee katika maisha ya Binti yake na kumtakia maisha mema yenye heri na
fanaka kwenye maisha yao baada ya kufunga ndoa.
Naye Mama Majinjah kama ilivyo desturi
kwa mzazi furaha yake ameionesha kwa kuendelea kumuombea dua njema mwanaye
akimtaka aendelee kujitunza na kulinda heshima ya mchumba wake hadi siku
itakapofungwa ndoa.
Marafiki wa karibu na familia hii
baba mdogo wa Tunsubilege Benjamin Mwandete ameelezea furaha yake na kuahidi
kusaidia kufanikisha ndoa hii ili iwe simulizi kwake na hata kwa mchumba wake.
Hii ni siku ambayo Tunsubilege
Kabungo Majinjah na mchumba wake Winfred Kamara walivikana pete za uchumba Mungu
wabariki Tunsubilege na Winfred kufikia siku hiyo itakayotengeneza historia nzuri
ya maisha yao.
0 Comments
Post a Comment