Naibu Waziri wa Maji
Mhandisi Maryprisca Mahundi amewaonya wananchi ambao wameng'oa mabango
yaliyowekwa na kuharibu alama za mipaka kwa ajili ya utunzaji wa chanzo cha
maji katika vijiji vya Chiwachiwa na Kisegese Wilaya ya Kilombero Mkoa wa
Morogoro.
Mahundi ametoa onyo
hilo katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Morogoro na kusikitishwa na
watu wasiojullikana walioharibu miundombinu ya mradi huo wenye gharama zaidi ya
shilingi bilioni tatu.
Amesema serikali
kupitia Rais Samia Suluhu Hassan imeelekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji
na kwamba Wizara haitavumilia uharibifu na kusema kuwa uchunguzi dhidi ya uharibifu huo umeanza
watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.
Eneo hilo la mto Lwipa lipo chini ya usimamizi wa bodi ya maji bonde la mto Rufiji ambao waliweka bikon mia mbili kuzunguka eneo hilo ikiwa ni ishara ya ukomo wa shughuli za kibinadamu lakini kundi la watu wasiofahamika wameng'oa bikoni mia moja themanini.
Amewataka wananchi kuilinda miundo mbinu ya maji kwani serikali inatumia fedha nyingi ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.
Mhandisi Aron Kilamba mkandarasi wa tanki la maji ameiomba jamii kuwa sehemu ya utekelezaji na walinzi wa mradi.
Mbunge wa Jimbo la
Mlimba Godfrey Kunambi ameishukuru serikali kwa kutatua changamoto iliyokuwa
inawakabili wananchi wake ya upatikanaji wa maji safi na salama Jimboni kwake.
0 Comments
Post a Comment