*SERIKALI KUHAMASISHA WAWEKEZAJI KUWEKEZA ENEO LA JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI-IPOLE TABORA*
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) Serikali itaendelea kuhamasisha wawekezaji kuwekeza katika maeneo ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Ipole, mbuga za Ipembampazi na Isuvangala Sikonge mkoani Tabora ili kuvutia watalii.
Ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Sikonge, Mhe. Joseph Kakunda aliyetaka kujua lini Serikali itajenga uwanja wa ndege wa Ipole na nyumba ya kupumzikia watalii wanaotembelea jumuiya hiyo kwa ajili ya utalii wa picha na kuangalia wanyama.
Amesema lengo la kuvutia wawekezaji kwenye maeneo hayo ni kuhakikisha watalii wanaotembelea jumuiya hiyo, mbuga za Ipembampazi na Isuvangala wanafika bila matatizo.
Aidha, amefafanua kuwa watalii wanaotembelea eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Ipole wanatumia uwanja wa ndege wa tabora na kiwanja kidogo cha Koga.
0 Comments
Post a Comment