RAIS SAMIA AZINDUA MRADI WA MAJI WA BIL 19,WAZIRI AWESO MHANDISI MARYPRISCA WASHIRIKI UZINDUZI.
RAIS Samia Suluhu Hassan amezindua mradi wa maji wa Chalinze- Mboga,mradi ambao umegharimu Shilingi Bilioni 19.
Katika hotuba yake Rais Samia amewataka wananchi wa Chalinze kuilinda miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ili iwe na manufaa kwa jamii.
Awali Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema Wizara imepokea fedha nyingi kutoka serikalini na kuwa wao kama watendaji, watahakikisha wanawajibika ipasavyo bila kumwangusha Rais.
Katika uzinduzi huo uliohusisha viongozi na watendaji mbalimbali wa serikali umehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi.




0 Comments
Post a Comment