UWT IRINGA YAJIVUNIA VIONGOZI WANAWAKE*
Umoja wa wanawake Tanzania UWT mkoa wa Iringa, leo umefanya kongamano la kumpongeza Rais wa JMT mama *SAMIA S.HASSAN* Kutokana na kazi azifanyazo na hivyo kuwatia moyo wanawake wote, pia Kongamano hilo lilitumika kumpongeza Spika wa bunge mhe *DR TULIA A.MWANSASU* Kwa kuchaguliwa kuwa spika wa bunge la JMT...
Mgeni rasmi kwenye kongamano hilo, mhe spika DR TULIA A.MWANSASU ambaye aliwakilishwa na mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mbeya, ambaye ni naibu waziri wa Maji, mhe eng *MARYPRISCA W.MAHUNDI* Amewashukuru wanawake wa UWT mkoa wa Iringa kwa kuthamini na kuenzi kazi zinazofanywa na viongozi katika kuwaletea maendeleo wananchi....
Pia aliwasihi kuendelea kushirikiana na serikali ili wao kama wenye ilani utekelezaji wake uwe mzuri....
Pia ameshukuru na kuwapongeza viongozi wa chama na serikali kwa jinsi wanavyoshirikiana kutekeleza ilani ya CCM ambayo walishirikiana kuinadi mbele ya watanzania...
Mungu ibariki Tanzania..
Mungu mbariki Mama SAMIA..
Mungu bariki viongozi wetu...
KAZI IENDELEEE💪🏻
0 Comments
Post a Comment