Kamishina wa Tume ya Maadili Jaji wa Rufani Sivangilwa Mwangesi akizungumza na watumishi wa Mkoa wa Mwanza katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma wakati Tume hiyo ilipokwenda kuzungumza kuhusiana na Maadili
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Gabriel Robart akizungumza wakati akimkaribisha Kamishina wa Tume ya Maadili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo katika wiki ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Kamishina wa Tume ya Maadili hayupo pichani wakati maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambapo Tume ya Maadili imekwenda kuwanoa kuhusiana na maadili.
Kamishina wa Tume ya Maadili Jaji wa Rufani Sivangilwa Mwangesi akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mwanza.
Na Mwandishi Wetu
Kamishna wa Tume ya Maadili Jaji wa Rufani Sivangilwa Mwangesi amewataka Viongozi wa Umma kufanya kazi kwa Uadilifu na kutojiingiza katika vitendo vinavyopelekea ukiukwaji wa Maadili.
Mwangesi ameyasema hayo katika Kikao chake na Viongozi wa Mkoa wa Mwanza katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16 hadi Juni 23 ambapo Ofisi Tume ya Maadili imefanya kikao na watumishi wa Mkoa wa Mwanza katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Mwangesi amewaasa Viongozi hao kitojiingiza katika mgongano wa Maslahi jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Ameongeza kuwa endapo viongozi watawajibika katika maeneo yao ya kazi kwa uadilifu itapelekea kujenga imani kwa wananchi wanaowaongoza na Serikali kwa ujumla.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amefafanua kuwa Maadili ni hatua muhimu inayo tambulisha mtu ndani ya Jamie husika na maadili hujitokeza katika matendo yake.
Mhandisi Robart ameongeza kuwa lengo la kikao hiki ni kuunga mkono jitiihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kupinga vitendo vya Rushwa, Ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za Umma.
Maadhimisho hayo ya Wiki ya Utumishi wa Umma nchini yameanza rasmi Leo Juni 16 na yatahitimishwa Junj 23, 2022
0 Comments
Post a Comment