NA KENNETH NGELESI,MBEYA


WATUMISHI wa Halmashauri ya jiji la Mbeya wamepongeza uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwaongezea asilimia ishirini na tatu (23%) ya mshahara kwa watumishi kima cha chini kwa vile ongezeko hilo litaleta usawa na kuchochea bidii kwenye utendaji kazi.


Akizungumza na waandishi wa Habari kwa niaba ya watumishi wa kaimu Mkurugenzi Triphonia Kisiga alisema watumishi kwa ujumla wao wanaishukuru Serikali Chini ya Mama Salia Suluhu Hassan kwa nyongeza ya mshahara ya asilimia 20 kwa watumishi wa kima cha chini na kwamba ameiongesha kujali na kuleta usawa katika ofisi.


Triphonia alisema watumishi waliongezewa mishahara ni kundi lenye watumishi wengi katika ofisi za Umma hivyo uamuzi wa Rais kujali kundi hilo ni wakizalengo kwani utachochea watumishi kufanya kazi kwa kujituma na kwa ufanisi katika kuwahudumia wananchi.


"Nitumie fursa hii kwa niaba ya watumishi kumshukuru Rais kuwaongezea mishahara hasa wale wa kima cha chini ,watumishiwa wote katika ofisi yangu wamefurahishwa hasa kwa ahadi yake ya ukweli katika kipindi kifupi tu" alisema Triphonia 


Alisema ongezeko hilo linakwenda muchochea watumishi wa ngazi zote kufanya kazi kwa bidii kwani hata sitofahamu iliyojitokea Waziri Mkuu Majaliwa Kassimu Majaliwa alishatolea ufafanuzi na watumishi wameelewa na wanaendelea kuachapa kazi.


" Tunashukuru kwa ufafanuzi wa waziri Mkuu Majaliwa Kasimi Majaliwa kwa kulitolea ufafanuzi hasa baada ya sitofahamu lakini kwa ujamla wao wameelewa ufafanuzi huo na wanaendelea kuchapa kazi kwa moyo wote" alisema Triaphone


Kwa Upende wake Meya wa Jiji alisema DorMohamed Issa alisema ongezeko hilo la mshahara linakwenda kuongeza morali kwa watumishi hivyo wanaamini kuwa sasa jiji litakwenda kuwa vizuri katika kika Sekta.


" Mimi kama mwakilishi wawachini nishukuru kwa Rais Kuongeza asilimia 20 wa watummishi wenye kima cha Chini itaongeza marali na imani yangu kazi itafanyika kwa ufanisi" alisema Mohamed Meya jiji la Mbeya