Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Angelina Ngalula (wa pili kushoto) na Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM, Rukia Yazid, wakizindua nembo kuashiria uzinduzi rasmi wa Siku ya Taasisi ya Delta Binafsi 2022 jijini Dar es Salaam leo.


Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Angelina Ngalula (wa tatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa  uzinduzi rasmi wa Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi 2022. Wengine ni viongozi wa TPSF na wawakilishi wa makampuni wadhamini

Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM, Rukia Yazid (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi wa Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi 2022. Wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa TPSF, Bi. Angelina Ngalula, viongozi wa TPSF na wawakilishi wa makampuni wadhamini.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Angelina Ngalula, akipokea mfano wa hundi ya shs 58,300,000 kutoka kwa Mkuu Uendeshaji wa Kundi la Makampuni ya Bravo, Group Evarist Maganga (wa pili kulia) ikiwa ni udhamini wa kampuni hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wake jijini Dar es Salaam leo.


Baadhi ya waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi jijini Dar es Salaam leo


Maadhimisho ya sekta binafsi kufanyika Jijini Dar Es Salaam wiki ya kwanza ya mwezi Disemba,2022.

 

Mwenyekiti wa Bodi ya sekta binafsi Tanzania Bi Angelina Ngalula amesema maadhimisho  wiki ya tathimini kwa sekta binafsi tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani itayoshirikisha wajumbe elfu moja kutoka Viongozi wa Kisekta,Wakurugenzi watendaji,Wafanyabiashara na Viongozi waandamizi yatafanyika Jijini Dar Es Salaam Ukumbi wa Superdome Arena Masaki wiki ya kwanza ya mwezi Disemba mwaka huu.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa Rais na Watanzania kufuatia ajali ya ndege iliyotokea Bukoba ambapo watu kumi na tisa wamepoteza ma isha na wengine kupata majeraha

 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari Bi Angelina amesema baadhi ya mambo yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na

1.  Kukuza uchumi licha ya janga la uviko-19 – Ukuaji wa uchumi nchini umekuwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita licha ya kuwepo janga la uviko 19.

2.  Kuifufua sekta ya Utalii nchini. Filamu ya The Royal Tour, Tumeona kutoka Januari hadi Julai 2022, jumla ya watalii 742,133 walitembelea Tanzania. Hili ni ongezeko la watalii 285,867, sawa na +62.7% ikilinganishwa na mwaka uliopita

3.  Kukuza Sekta ya kilimo kupitia mikopo nafuu: Baada ya maelekezo ya Mhe Rais ya kushusha riba kwenye sekta ya kilimo, tumeshudia benki zetu kushusha riba kwa mfano CRDB ilishushakutoka 20% mpaka 9%, NMB 10% mpaka 9%, TADB 11% to 9% hivyo kuwezesha wadau wa kilimo kupata mikopo kwa unafaano kukuza sekta ya kilimo sambamba na Ajenda 10/30.

4.  Kuridhia Mkataba wa kujiunga na Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA). Tanzania imechaguliwa kati ya nchi nane kuanza  kuuza bidhaa zake k atika Eneo hili hakuhukuwa kinufaika na pungozo za kodi. Kama Sekta binafsi tumejiandaa kuhakikisha tunawekeza kwenye viwanda ili wafanyabishara wetu wasafirishe mizigo yao nje ya nchi.

5.  KufunguamasokoyaKimataifa – Mhe Rais amefanya kazi kubwa sana kufungua