Afisa Masoko Mwandamizi wa Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kelvin akiongea na wananchi,wadau juu ya umuhimu wa kutunza mazingira.
Maulid Nsalamba na Gabriel Manase wote ni Afisa Mkaguzi na mdhibiti wa vyombo vya majini wakitoa Elimu kwa wananchi. Ulinzi Usalama na Utunzaji wa Mazingira
Wananchi wakiwa makini kuwasikiliza
Amina Miruko- afisa uhusiano mwandamizi
akiwa na maafisa wenzake wakiendelea na zoezi la kutoa Elimu kwa Wananchi
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa elimu ya ulinzi, usalama na utunzaji wa mazingira kwa wananchi mbalimbali katika wilaya ya Ifakara Mkoani Morogoro kwa lengo la kuwajengea uelewa wananchi hao katika maeneo hayo.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mafunzo hayo Novemba 13,2022, Afisa Ukaguzi na Mdhibiti wa vyombo vya majini wa TASAC Bw. Gabriel Manase amesema kuwa zoezi hilo lilianza Novemba 11, 2022 Ifakara Mkoani Morogoro na kwamba litaendelea katika mikoa mingine ya Iringa na Dodoma.
“Zoezi hili ni endelevu lilianza hapa Ifaraka Novemba 11, mwaka huu katika maeneo ya, Ngalimila, Ngapemba, Utengule, Chita, Mngeta na Mchombe, na linaendelea katika mikoa ya iringa na Dodoma” amesema Manase.
Shirika hilo limekuwa na desturi ya kutoa elimu juu ya masuala mbalimbali yakiwemo ulinzi, usalama na utunzaji mazingira kwa wananchi wanaotumia vyombo vya majini pamoja na wale wanaofanya shughuli zao za kiuchumi majini kwa kuhakikisha wanapata uelewa wa kutosha ili elimu hiyo iwasaidie wanapokuwa kwenye majukumu yao ya kila siku wanapotumia vyombo vya usafiri majini.
Aidha, TASAC wameendesha zoezi la ukaguzi wa vyombo vya usafiri majini vinavyotumika katika eneo hilo.
Huo umekuwa ni muendelezo kwa TASAC kukutana na wananchi katika maeneo mbalimbali na kuwapa elimu kwa kuhakikisha kunakuwepo na ulinzi, usalama na utunzaji mazingira, katika maeneo yote ya bahari, maziwa, mito na mabwawa.
0 Comments
Post a Comment