Mkuu wa chuo akizungumza katika mahafali hayo
Sehemu ya wazazi na walezi wa wahitimu
Sehemu ya wanafunzi wa kike wanaochukua somo la TEHAMA
Mgeni rasmi
Sehemu ya wanafunzi wa somo la umeme wakionyesha umahiri wao kwa wazazi
MAHAFALI YA 9 CHUO CHA VETA MULEBA YAFANA , UONGOZI WAIOMBA SERIKALI JUU YA KUPANDA GHARAMA ZA MAISHA.
Na Lydia Lugakila Kagera
Chuo cha Muleba Rutheran vocational Training Center (MLVTC) kilichopo mkoani Kagera kimefanikiwa kuhitimisha vijana 19 katika mahafali ya tisa, huku uongozi wa chuo hicho ukiililia serikali juu ya kupanda kwa gharama za maisha hasa katika ununuzi wa vifaa vya kufundishia pamoja na chakula cha wanafunzi.
Akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika katika chuo hicho mkuu wa chuo Goldian Nteboya amesema kuwa licha ya jitihada zilizopo kati ya chuo na serikali katika kuhakikisha wanawasaidia vijana kuwaongezea uwezo wa kujiari na kupunguza utegemezi kwa wazazi bado uongozi huo bado unashindwa kufikiria kuongeza ada kutokana na ada kulipwa kwa shida kutokana na kupanda gharama za maisha.
Nteboya amesema kuwa misaada mkubwa katika jambo hilo wanaitegemea sana serikali ili bei za bidhaa zishuke na kutengemaa.
Katika lisala ya wahitimu iliyosomwa na Janeti Gidion mbele ya mgeni rasmi imeeleza kuwa malengo ya serikali na watengenezaji wa sera ya Tanzania ya viwanda kwa ajili ya watanzania wote kutokana na ukosefu wa ajira wataalam wengi hawanufaiki na taaluma inayotolewa katika chuo hicho hadi kusababisha wengi wao kuishia kufanya shughuli nyingine ambazo ni tofauti kile walichokisomea, kukosa baadhi ya vitendea kazi kwa ajili ya masomo yao, ufinyu wa darasa la umeme, upungufu wa vifaa vya matengenezo kwa upande wa tehama na umeme.
Kufuatana na hali hiyo wahitimu hao wameiomba serikali kutoa ajira pindi wanapomaliza muda wao wa mafunzo ikiwa ni pamoja na kutolewa kwa mikopo kwa wahitimu hao ili wajiajiri wenyewe.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika mahafali hayo Dikson Mnyaga ambaye ni
Afisa Biashara kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Muleba amekiri kuwepo kwa ajira chache hivyo amewaomba wahitimu hao kutumia vyama somo la stadi za maisha kuwa wabunifu, kuanzisha biashara zao ili wajipatie kipato, wasisite kujiendeleza kupambana na tatizo la ajira.
Hata hivyo chuo hicho kilianzishwa tangu mwaka 2012 ambapo wahitimu hao wamejifunza masomo yakiwemo ya TEHAMA, umeme, ujasiriamali, stadi za maisha, na mengineyo.







0 Comments
Post a Comment