Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe ameitaka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kujikita katika Ubingwa bobezi na Tiba Utalii na kuwa chanzo za fedha za kigeni katika lango kuu la ukanda wa Nchi za SADC.Dkt. Magembe ametoa kauli hiyo Jijini Mbeya wakati akifanya majumuisho ya ziara yake katika Mkoa huo ambapo amesema kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA KUJIKITA KATIKA UBINGWA BOBEZI NA TIBA UTALII
Na. WAF, Mbeya
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe ameitaka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kujikita katika Ubingwa bobezi na Tiba Utalii na kuwa chanzo za fedha za kigeni katika lango kuu la ukanda wa Nchi za SADC.
Dkt. Magembe ametoa kauli hiyo Jijini Mbeya wakati akifanya majumuisho ya ziara yake katika Mkoa huo ambapo amesema kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Tunakila sababu ya kujikita katika Tiba ya Utalii kwani tupo imara kuanzia wataalamu, miundombinu, vifaa na vifaa tiba pamoja na dawa na vitendanishi”, amesisitiza Dkt. Magembe
Ameeleza kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika utoaji wa huduma za afya hasa huduma za ubingwa na ubingwa bobezi.
Ameongeza kuwa pamoja na kutoa huduma za ubingwa na ubingwa bobezi anataka rufaa zote katika nchi za lango kuu la ukanda wan chi za SADIC zije Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.
“Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya ni miongoni mwa Hospitali zilipo katika mpango maalum wa kuanzishiwa wa huduma ya matibabu ya mionzi kwa wagonjwa wa saratani.
Vile vile amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.
Aidha, Dkt. Grace ametoa wito kwa Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya na Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya kuweka utaratibu wa kuzijengea uwezo kwenye Hospitali za Wilaya, Zahanati na Vituo vya Afya kwa lengo la kuwaongezea ujuzi watumishi katika ngazi ya msingi.
Amesema kuwa ujuzi huo utasaidia kuendanda na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali kwenye sekta ya afya.
Dkt. Grace Amesema kuwa amefurahishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa Ujenzi wa Jengo la Huduma ya Afya ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.
Hata hivyo amewataka viongozi wa Mkoa wa Mbeya kujenga ushirikiano ili kuhakikisha mwananchi anapata huduma bora kwa wakati.
Amehitimisha kwa kusisitiza viongozi wa Mkoa huo kuwa na utamaduni wa vikao na watumishi wao vya mara kwa mara kwa lengo la kuwasikiliza na kutatua changamoto zao ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.
0 Comments
Post a Comment