Uongozi wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) chafanya Thathimini ya uwanja wa Medani Mkomazi.

Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi- Mkomazi Tanga

Uongozi wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) Pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga wametembelea Uwanja wa mbinu za medani ya kivita kwa ajili ya maandalizi ya mafunzo kwa maofisa wananfunzi na wakaguzi wasaidizi wa Polisi eneo la Mkomazi wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.

Akiongea katika uwanja wa mbinu medani Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dk Lazaro Mambosasa amesema eneo hilo ni maalum kwa mafunzo ya Medani za kivita kwa maofisa wa Jeshi la Polisi ambao wapo katika mafunzo ya Jeshi hilo.

Dk Mambosasa ameongeza kuwa lengo la ziara hiyo ni kwa ajili ya maandalizi ya mafunzo ya mbinu za medani kwa wanafunzi wa kozi ya uofisa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi yanayotarajiwa kufanyika siku za hivi karibuni amebainisha kuwa katika kuhakikisha hilo linafanikiwa kumekuwepo na changamoto ya chanzo cha maji katika eneo hilo kwa ajili ya askari wanaokuwa katika mafunzo na wananchi wanaozunguka pori hilo.

Ameongeza kuwa kutokana na changamoto hiyo wananchi wa Mkoa wa Tanga wamejitolea kuchimba kisima cha maji safi kwa ajili ya matumizi ya askari wanaokuwa mafunzoni ili kuongeza ufanisi kwa mafunzo hayo kwa maofisa hao wanafunzi na wakaguzi wasaidizi wa Polisi.

Akiongea kwa niaba ya wananchi wenzake Balozi wa maji Mkoa wa Tanga Habibu Mbota ameahidi kuchimba kisima cha maji safi katika kuboresha mafunzo hayo na vijiji jirani venye wakazi zaidi ya elfu tano (5000) kuunga  mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ambayo inaongozwa na mheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya  kufikisha huduma kwa wannchi.