Katibu Mkuu Kiongozi Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said
katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Udhibiti
Ununuzi wa Umma (PPRA) Dkt. Leonada Mwagike kushoto, akiwa na Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar
(ZPPDA) Dkt. Sharifa Omar Salim walipomtembelea ofisini kwake leo.
Katibu Mkuu Kiongozi Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said
katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PPRA Dkt. Leonada
Mwagike na Afisa Mtendaji Mkuu PPRA Bw. Eliakim Maswi (kushoto), pamoja na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi (ZPPDA) Dkt. Sharifa na Mkurugenzi Mtendaji
ZPPDA Bw. Othman Juma Othman walipomtembelea ofisini kwake leo.
ZAWADI MSALLA- ZANZIBARI
Katibu Mkuu Kiongozi wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhe. mhandisi Zena Ahmed Said
amewataka Taasisi zinazosimamia ununuzi wa Umma nchini Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa
Umma (PPRA) na Mamlaka ya Ununuzi na uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar (ZPPDA)
kuhakikisha wanatoa mafunzo ya Sheria ya Ununuzi ipasavyo kwa watendaji wakuu wa Serikali
ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi wakati wa utekelezaji wa michakato ya ununuzi.
Mhandisi Zena ameyasema hayo leo alipokutana na bodi za Wakurugezi na menejmenti za
Taasisi hizo mbili ofisini kwake Ikulu Zanzibar. Ameeleza kuwa eneo la ununuzi Serikalini ni kati
ya aeneo lenye changamoto na linalohitaji kutolewa mafunzo ili kuhakikisha thamani ya fedha
katika ununuzi inapatikana.
Amesema kuwa watendaji wakuu wa taasisi wanatakiwa kuhakikisha taratibu za ununuzi
zinafuatwa na kuufahamu vizuri mchakato mzima wa ununuzi. Hii itasaidia katika kuhakikisha
ununuzi unafanyika kwa haki, uwazi na thamani ya fedha inaonekana kwani zaidi ya asilimia
sabini ya bajeti ya Serikali zote mbili imeelekezwa katika ununuzi.
“Watendaji wakuu wengi wamekuwa wakishindwa kufuata taratibu za michakato ya ununuzi hii
ni kazi yenu kuhakikisha mnawapatia mafunzo stahiki ili kusaidia matumizi mazuri ya fadha ya
Setrikali” Alieleza.
Pia, Mhandisi Zena amesema mafunzo hayo yanatakiwa kutolewa kwa bodi za zabuni ili
kuhakikisha bodi hizo zinapitisha manunuzi kwa kufuata sheria ya ununuzi wa Umma na kanuni
zake na kuelewa kitu wanacho kipitisha. Ameongeza kuwa bodi hizo za zabuni ni muhimu
kusisitiziwa umuhimu wa kusoma nyaraka zote za zabuni kabla ya kupitisha zabuni yoyote.
Aidha, Mhandisi Zena aliitaka PPRA kuhakikisha inasaidiana kwa ukaribu na ZPPDA katika
mambo mbalimbali ili kuhakikisha Taasisi hiyo inakuwa kati ya Taasisi bora kwa upande wa
Tanzania Zanzibar. Alisema anatambua PPRA ni Taasisi kongwe kidogo ukilinganisha na ZPPDA
na tayari imeshaisaidia Serikali kwa kiwango kikubwa katika masuala ya ununuzi.
“Nina fahamu hapo zamani PPRA mlikuwa mkitoa mafunzo, nina amini mpaka sasa bado
mnatoa mafunzo, wapeni mbinu hizo ZPPDA za utoaji wa mafunzo, mmenieleza mmejinge
mfumo mpya wa ununuzi ni wakati muafaka kwa ZPPDA Kwenda kujifunza na kuona ubora wa
mfumo huo, ili walinganishe na mfumo walio nao na wanaoutumia kwa sasa” Alisema
Kwa upande wa PPRA mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Dkt. Leonada Mwagike alimueleza
Mhandisi Zena kuwa PPRA imejipanga kushirikiana na ZPPDA na ndiyo lengo kuu lililowafanya
waweze kufika Zanzibar. Dkt. Mwagike alieleza kuwa tayari Taasisi hizo mbili zimeweka
maazimio ya kusaini mkataba wa mashirikiano ambapo unatarajiwa kusainiwa ndani ya miezi
mitatu kuanzia sasa.
Dkt. Mwagike alieleza mkataba huo utaangalia vipengele vyote muhimu vya utendaji ikiwemo
kubadilishana uzoefu kwa watumishi wa Taasisi hizo mbili na kubadilishana ujuzi wa kutoa
mafunzo ya sheria ya ununuzi wa umma.
Naye Mwenyekiti wa ZPPDA Dkt Sharifa Omar Salim alisema ujio wa Taasisi mwenza umeleta
hari kubwa kwa upande wao na kuongeza kuwa wanaanimi mkataba watakao enda kuingia kati
ya Taasisi hizi mbili utazaa matunda.
“Licha ya kwamba tayari Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu
Hassan alizitaka Taasisi zinazofanana kwa pande zote mbili kushirikiana sisi ZPPDA tumeona
upendo na shauku waliyo nayo PPRA kuhakikisha taasisi zetu zinasonga mbele” Alisema
0 Comments
Post a Comment