Naibu Waziri wa Maji, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), amewahakikishia huduma ya majisafi na salama kwa wakazi 3600 wa vijiji Kitanda na Mgwangala kupitia mradi wa maji wa Kitanda ambapo utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 98 na wananchi wanapata huduma ya majisafi. Mradi huo umetekelezwa ndani ya miezi 6 kwa gharama ya shilingi Milioni 473.1 na kazi zilifanyika ni pamoja na Ujenzi wa tenki la lita laki 150; Uchimbaji na ulazaji wa mabomba umbali wa kilomita 19.9; Ujenzi wa vituo 14 vya kuchotea maji.

 Mhe. Maryprisca Mahundi amesema hayo akiwa katika ziara ya kikazi ya Ndugu. Mary Pius Chatanda Mwenyekiti UWT Taifa Mkoani Ruvuma ambapo aliweza Kutembelea na kukagua utekelezaji wa 

mradi wa maji wa Kitanda. Mhe. Mahundi amesema kwa vijiji lupilo na Masimeli ambavyo usanifu umekamilika na ujenzi utaanza kadri ya upatikanaji wa fedha

*Vijiji vya Kitanda na Mgwangala vilivyopo kata ya Kitanda kupata huduma ya majisafi*  

 *27 Julai, 2023* (Mbinga-Ruvuma)

Naibu Waziri wa Maji, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), amewahakikishia huduma ya majisafi na salama kwa wakazi 3600 wa vijiji Kitanda na Mgwangala kupitia mradi wa maji wa Kitanda ambapo utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 98 na wananchi wanapata huduma ya majisafi. Mradi huo umetekelezwa ndani ya miezi 6 kwa gharama ya shilingi Milioni 473.1 na kazi zilifanyika ni pamoja na Ujenzi wa tenki la lita laki 150; Uchimbaji na ulazaji wa mabomba umbali wa kilomita 19.9; Ujenzi wa vituo 14 vya kuchotea maji.

Mhe. Maryprisca Mahundi amesema hayo akiwa katika ziara ya kikazi ya Ndugu. Mary Pius Chatanda Mwenyekiti UWT Taifa Mkoani Ruvuma ambapo aliweza Kutembelea na kukagua utekelezaji wa 

mradi wa maji wa Kitanda. Mhe. Mahundi amesema kwa vijiji lupilo na Masimeli ambavyo usanifu umekamilika na ujenzi utaanza kadri ya upatikanaji wa fedha 

Kwa upande wa Mheshimiwa Jonas Mbunda Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini ameishukru Wizara kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa miradi ya maji katika Jimbo la Mbinga Mjini ambapo ameeleza kuwa  Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi *nane (8)* kwa gharama zaidi *billion 5.8*

Aidha, Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Mary Pius Chatanda amesisitiza wananchi wa  kijiji cha kitanda waendelea kutunza na kuhifadhi chanzo cha maji kwa kupanda miti rafiki