Katika kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya leo tarehe 19 Oktoba, 2023 imezindua jengo jipya la kutolea huduma ya Tiba Mazoezi (Fiziotherapia) kwaajili ya kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa wenye matatizo ya maumivu ya viungo.

Akiongea wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa Jengo hilo Dkt. Godlove Mbwanji Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, ameushukuru uongozi wa hospitali pamoja kamati yote iliyofanikisha kukamilika kwa jengo hilo pamoja na ushirikiano ulioonyeshwa na watumishi wa hospitali akiwemo Mhandisi alisiyesimamia shughuli zote za ujenzi huo.

“..na mimi naomba shukrani zote nilizopewa ni za uongozi wa hospitali na watumishi wote kwasababu vyote vilivyofanyika ni watumishi wamefanya kazi kupitia sehemu ya mapato yanayopatikana..” – Dkt Mbwanji

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YAZINDUA JENGO JIPYA LA TIBA MAZOEZI

Aidha ametoa rai kwa watumishi wa idara hiyo inayohusika na huduma ya Tiba mazoezi  kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kufanya mazoezi ili kuepukana na magonjwa yasiyo ya lazima.

Seraphine Mushi ni mkuu wa idara ya fiziotherapia hospitalini hapa, ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya chini ya Dkt. Mbwaji kupitia maboresho mbalimbali yaliyofanyika katika idara hiyo ikiwemo ongezeko la vifaa tiba pamoja na upanuzi wa jengo hilo ambapo hapo awali lilikuwa na uwezo kuhudumia wagonjwa wa nje 30 hadi 40 kwa siku na sasa lina uwezo wa kuhudumia wagonjwa wa nje zaidi ya 120 hadi 200 kwa siku. 

“…hapo awali jengo hili lilikuwa na vyumba 16 vya matibabu na sasa vimeongezeka vyumba nane pamoja na eneo la kufanyia mazoezi ambavyo vitapelekea uwezo wa kutibu wagongwa wa nje 120 hadi 200 kwa siku ukilinganisha na zamani tulikuwa tukiona wagonjwa 30 hadi 40 kwa siku..” – Seraphine Mushi

Mathias Mkoma, Revocatus Zege na Mitreni Sichembe ni wagonjwa wanaopatiwa huduma ya matibabu kwa njia ya tiba mazoezi Hospitali hapo wamepongeza uongozi wa hospitali pamoja na watumishi wa idara hiyo kutokana na  huduma wanazopatiwa katika kipindi chote cha huduma.

“..tumefurahishwa sana na huduma zinazopatikana katika idara hii hivyo hatuna budi kuupongeza sana uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, wahudumu wote pamoja na madaktari kwa kweli wanafanya kazi kwa upendo sana…” 

Katika hafla hiyo pia watumishi kutoka idara ya Fiziotherapia walipata nafasi ya kumkabidhi Cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji kama ishara ya kutambua mchango wake kutokana na ushirikiano mkubwa anao uonyesha katika jitihada mbalimbali za kuboresha huduma hospitalini hapo kitendo kilichoambatana na zoezi la ukukataji wa keki kama ishara ya pongezi.