Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Claudia Kitta amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia hospitali ya Wilaya jumla ya shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya majengo na vifaa tiba ambapo sasa hospitali imeanza kutoa huduma mbalimbali zikiwemo za upasuaji.

Kitta ameyasema hayo wakati akitembelea kambi ya macho maalum kwa ajili ya matibabu ya mtoto wa jicho yaliyofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Helen Keller International kwa ushirikiano na Wizara ya Afya.

"Kipekee nimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuifanya Wilaya kuwa na hospitali ya Wilaya kwani wananchi wengi walikuwa wakienda kutibiwa Ilembula,Njombe na Mbeya ambapo wanatumia gharama kubwa sana"alisema Kitta.

Naye Dkt Barnabas Mshangila Daktari bingwa wa macho kutoka hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya amesema siku tatu za mwanzo wamefanya upasuaji wagonjwa mia moja themanini na tano na wamepata matokeo mazuri.

Amesema hivi sass huduma mbalimbali zimeanza kutolewa kama kujifungua na wagonjwa wa dharula.

"Kipekee nimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuifanya Wilaya kuwa na hospitali ya Wilaya kwani wananchi wengi walikuwa wakienda kutibiwa Ilembula,Njombe na Mbeya ambapo wanatumia gharama kubwa sana"alisema Kitta.

Hospitali imekuwa na majengo ya kisasa na vifaa bora hata kuwezesha matibabu ya kibingwa kufanyika kwa mara ya kwanza Wilaya ya Wanging'ombe.

Kwa upande wake Dkt Sarah Ludovick mwakilishi wa Wizara ya Afya mesema Wizara inaendelea kusomesha madaktari wa macho ili huduma za kibingwa ziweze kutolewa wilayani hivyo kuwapunguzia makali wananchi wa kipato cha chini.

Aidha amesema tatizo la mtoto wa jicho ni kubwa nchini ambalo zaidi huwakumba wazee ambao wengi wao hawana kipato na hupoteza uoni baadhi wamekuwa vipofu kutokana na ukosefu wa kipato.

Naye Dkt Barnabas Mshangila Daktari bingwa wa macho kutoka hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya amesema siku tatu za mwanzo wamefanya upasuaji wagonjwa mia moja themanini na tano na wamepata matokeo mazuri.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Wwanging'ombe Dkt Frank Chiduo amesema wagonjwa wa mtoto wa jicho katika wilaya yake ni wengi lakini wengi wao hushindwa kufika hospitali kutokana na kukosa pesa za matibabu.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Wilaya Dkt Majaliwa Alphonce Chumvi amesema wagonjwa wote wanaopatiwa matibabu hulazwa wodini na hii ni kambi ya kwanza ya mtoto wa jicho kufanyika hospitalini hapo.

Kambi hii itasaidia kuitangaza hospitali kwani wagonjwa wametoka katika kata mbalimbali za wilaya ya Wanging'ombe.

Athuman Tawakal ni Meneja Mradi wa shirika la Helen Keller amesema shirika lake linatoa huduma katika mikoa ya Mbeya,Songwe na Njombe na kambi ya Njombe ni ya kwanza kufanyika lengo ni kuwafikia wagonjwa zaidi ya mia tatu.

"Shirika linawagharamia wagonhwa usafiri wa kwenda na kurudi kambi ya matibabu,chakula na gharama zote za matibabu"alisema Athuman.

Ameishukuru serikali pamoja na Wizara ya Afya kwa ushirikiano mzuri hata kuwawezesha kutekeleza majukumu yao bila mkwamo.

Hata hivyo shirika huwajengea uwezo maktari ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na hata mradi ukiisha muda wake tiba za mtoto wa jicho ziendelee kutolewa lengo ni kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini ambao hawaezi kusafiri wala kugharamia matibabu.

Enock Ngavatula(87)mkazi wa Lugodo ameishukuru serikali kwa kumuwezesha kupatiwa matibabu bure binafsi asingeweza kugharamia matibabu kutokana na ukosefu wa fedha.

Ni miaka miwili Enock alipoteza uwezo wa kuona hivyo shughuli za kiuchumi zilikwama na alikuwa mzigo kwa familia kutokana na utegemezi wa kila kitu.

Naye Kundi Masanganya(67)mkazi wa Mbalino Wilaya ya Mbarali amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea hospitali na kuwapatia matibabu ya mtoto wa jicho bila gharama yoyote.

Kambi nyingine ya mtot wa jicho itafanyika hivi karibuni Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe.