Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) Khadija Mwenda akizungumza na Jukuu la Wahariri (TEF) na Waandishi wa Habari kuhusiana na mafanikio ya OSHA kwa miaka mitatu ya awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mwenyekiti Jane Mihanji akitoa maelezo kuhusiana na ushiriki wa wahariri katika kikao kati ya OSHA na TEF jijini Dar es Salaam.

Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri akizungumza kuhusiana na uratibu wa Ofisi hiyo kwa Taasisi zilizo chini ya Msajili kueleza juu ya ufanisi wa kazi zao ,jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari katika mkutano kati ya TEF na OSHA jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu 


 Wakala wa Usalama Mahala Pa kazi (OSHA) imefuta tozo za ada 10 zenye thamani ya Sh.Bilioni 35 ambazo fedha hizo ilikuwa ikipata kila mwaka ikiwa ni kupunguza mzigo kwa wawekezaji kuhusiana na kulipia tozo.

Hayo ameyasema Mtendaji Mkuu wa OSHA  Khadija Mwenda wakati akizungumza katika kikao cha Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Waandishi wa Habari kwa uratibu wa Ofisi ya Masjili wa Hazina kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwenda amesema kuwa  katika mafanikio ya Miaka mitatu ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan baada kutoa tozo hizo  OSHA haijaweza kuteteleka lengo ni kuhakikisha nchi inapata wawekezaji wengi ambao watachochea uchumi na ajira kwa watazania.

"Baada kupunguza na kuondoa baadhi ya ada za huduma ambazo haujaadhiri usimamizi na utoaji wa huduma za usalama wa afya mahali pa kazi nchini," amesema  Mwenda.

Amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefungua mipaka ya uwekezaji nchini hivyo OSHA kazi yake ni kuendana na Rais katika kuhakikisha adhima ya Rais Wetu inatimia inayoendana na vitendo vya watendaji wake.

Aidha amesema OSHA inaangalia usalama mahala pa kazi kwa kipindi cha miaka mitatu wameweza kufanya ukaguzi katika maeneo ya kazi  yote na kuwapa cheti.

Amesema mafanikio  ya Wakala katika kipindi cha miaka  mitatu kuanzia mwaka 2021 hadi  2023 kuhimarika kwa shuhuli za usimamizi mahala pa kazi nchini  ambapo wakala amefanikiwa kuongea idadi ya maeneo ya kazi yaliyo sajiliwa kutoka 4336 hadi 30306 ongezeko hilo sawa na asilimia 599.

Mwenda amesema  OSHA kwa kushirikiana na wadau  wanaanda mpango  wa kutambua matumizi ya simu kwenye  vituo vya mafuta si salama  wanahitaji kutoa elimu zaidi namna ya kuboresha utoaji huduma juu ya malipo ya simu kwenye vituo hivyo.

"Kushirikiana na wadau kutengeneza  mpango wa kutambua  matumizi  ya simu kwenye vituo vya mafuta si salama kwa kutengeneza vibonzo kwa ajili elimu zaidi  watu waelewe sii salama  kazi  yetu kubwa  osha ni kuzuia na kutoa elimu, "amesema Mwenda.

Amesema   Dkt.Samia Suluhu Hassan amekuwa  akifanya juhudi kuhakikisha kuwa wawekezaji  wanakuja kuweza nchini  ikiwemo kuhimiza  uboreshaji  wa mazingira ya biashara  kuwa wezeshi na hili ni pamoja  na maelekezo  mbalimbali katika hotuba zake. 

Amesema  kuwa wao kama OSHA  wamefanya mapitio ya mlolongo wa shughuli  zao wa kuweza kubaini  maeneo yanayohitaji maboresho  katika utoaji wa  huduma  katika kulinda afya na usalama mahala pa kazi 


"Baada yakufanya na kujiridhisha kwa  mapitio hayo  tukakuta kuna maeneo  yanahitaji  maboresho  ambapo miongoni mwa maeneo yaliyoonekana kuwa na uhitaji wa maboresho tunafanya utatuzi katika  kufanya sehemu za kazi zinakuwa salama ili kuwa na uzalishaji wa nguvu kazi unakuwa unatija kwa Taifa".Amesema Mwenda 

Amesema ada zilizofutwa  ama kupunguzwa na OSHA zimeleta unafuu ambao unachochea ukuaji wa biashara na uwekezaji nchini ikiwemo Kuongeza ajira kwa watanzania.

Ameeleza kuwa kiasi cha ada zilizopunguzwa zinakadiriwa kuwa zaidi ya bilioni 35 ambapo imependeza Rais Dk.Samia  fedha  hizo zitatumika katika kuhimarisha mifumo  ya kulinda wafanyakazi waweze kuzalisha kwa tija.

Hata hivyo amesema idadi ya ukaguzi zilizofanyika zimeongezeka kutoka kaguzi 104,203 hadi kufikia kaguzi 776,968 sawa na asilimia 646 kaguzi hizo zilizohusisha ukaguzi wa jumla.

Amesema Taasisi ya OSHA amefanikiwa  kusimika mfumo wa TEHAMA  wa usimamizi wa taarifa  za kaguzi nchini  ambapo kupitia  mfumo huo huduma ya utoaji wa taarifa  za ukaguzi ajali na mfumo unafanyika kwa njia ya kieletroniki.

Mwenda  akizungumza kuhusu  changamoto zinazowakabili amesema baadhi ya waajiri kutotekeleza ipasavyo sheria namba 5 ya usalama na afya mahala pa kazi  wanaosimamia ikiwemo kuto wasilisha taarifa za ajali zinazotokea maeneo ya kazi. 

Amesema,  katiba ya nchi inasema kila binadamu  ana haki ya kuishi inatambua  hilo na wana  program kila maeneo  wanafikia kutoa elimu kulinda vijana. 

Amesema OSHA imekuwa kimbilio kwa nchi nyingine kujifunza  na hiyo kutokana kuwa mifumo thabiti ya utoaji huduma kuwa umetukuka pamoja na kupata kutambulika kimataifa pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO).


Mwishooo