Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,  Mohammed Khamis Abdulla  akipiga makofi akiwa na Watendaji wa TCRA, Mwenyekiti wa Bodi pamoja na wageni waalikwa mara baada ya kuzindua kitabu cha Kidijiti , jijini Dar es Salaam.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,  Mohammed Khamis Abdulla akipata maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) Khamis Mohd Ndogo kuhusiana na Teknolojia ya Ufugaji Kuku kwa Kutumia Tehama namna ya kupata taarifa katika banda katika Maonesho ya Mabanda kuhusiana ubunifu wa Kidijiti katika hafla ya uzinduzi Kitabu cha Kidijiti uliofanyika jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,  Mohammed Khamis Abdulla akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Klabu za kidijiti katika Shule za Msingi, Sekondari na vyuo Vikuu katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wanafunzi wakiimba wimbo wa Taifa katika hafla ya uzinduzi wa Kidijiti , jijini Dar es Salaam.



Na Mwandishi Wetu 


KATIBU Mkuu Wizara ya Habari  Mawasiliano na  Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla ametoa wito kwa wadau wa TEHAMA wakiwemo wakuu wa shule za awali msingi na sekondari pamoja na vyuo wahamasike kuanzisha  klabu za kidijiti lakini wahakikishe wanafuata misingi na maadili ya nchi.

Akizungumza novemba 2,jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kitabu Cha uwanzishwaji na uratibu wa Klabu za kidijiti amesema kuanzishwa kwa kitabu hicho ni muongozo wa vijana kupata fursa ya mapinduzi ya kidijiti.

Katibu Mkuu amesema ,kupitia kitabu hicho kitaleta dira chanya ya  ubunifu kwenye nchi katika mazingira ya sasa ambayo teknolojia ya Tehama inakua kwa kasi kwenye mifumo ya taarifa na uchumi.

"Sera ya mwaka 2016 ipo kwenye mchakato wa Kubadilishwa ambapo katika  mchakato huo tumeweka kipengele cha  kuchochea ntalanta na kuandaa sera ya kampuni changa ambayo itawasaidia baadaye kuwa na wadau wakubwa,"amesema

Amesema kujenga Taifa la kidijitali kupitia Klabu hizo zitachangia ufumbuzi na kuwawezesha vijana kuwa wabunifu na wajasiliamali kupotia TEHAMA.

Pia amesema uwanzishaji wa vituo vya ubunifu nchi nzima bila  kujali elimu waliyonayo kutasaidia kuongeza ajira nchini.

"Kwa Kujifunza TEHAMA itawasaidia kuwa Bora zàidi na kukuza uchumi na kusaidia mikakati ya kukuza uchumi,"amesema

Hata hivyo amesema Wizara itaongoza safari hiyo ya kidijitali ili nchi ifike katika uchumi ya kidijiti.

 Awali Mkurugenzi Mkuu TCRA Dkt.Jabir Bakari amesema klabu za kidijiti ni majukwaa ya hiari yanayowakutanisha wanafunzi wa rika moja kupata uelewa na kuhamasishana juu ya tehama uchumi kidijiti na fursa zake.

"Kupitia klabu hizi za kidijiti tunajenga jamii yenye ufahamu wa teknolojia ya kidijiti na iliyo na taarifa na fursa zake "amesema Dkt Bakari 

Dkt Bakari amesema lengo la uwekezaji kwenye tehama ni kuboresha na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma Kwa wananchi na kuongeza uwezo wa wananchi kushiriki kikamilifu katika uchumi kidijiti.

Ameongeza kuwa dunia ipo katika zama za taarifa zinazoenda sambamba na uchumi wa kidijiti .

"Katika zama hizi ambazo zinajulikana kama zama za mapinduzi ya nne ya viwanda tehama ndiyo nyazo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.