Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha ambazo zimewezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya màji.
Wizara ya Màji yaahidi kufikia lengo kwa wakati
Naibu Waziri wa Màji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema huduma ya maji hapa nchini imefanikiwa kwa sababu ya juhudi kubwa inayofanywa na Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo muhimu nchini.
Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha ambazo zimewezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya màji.
Mhe. Mahundi ametoa shukran hizo akiwasilisha taarifa ya hali ya upatikanaji wa fedha na utekelezaji kwa niaba ya Waziri wa Màji kwa kipindi cha nusu mwaka cha Julai - Desemba 2023.
Taarifa hiyo ameiwasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Màji na Mazingira ambapo Wizara imeendelea na utekekezaji wa miradi sehemu mbalimbali nchini na hayo yote yamewezekana kupitia nia ya dhati ya Rais Samia katika kuhakikisha ‘anamtua mama wa Tanzania ndoo ya màji’.
Amesisitiza kuwa lengo la Wizara ya Maji ni kumfikishia huduma ya màjisafi kila Mtanzania kwa wakati.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Màji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga (Mb)ameishukuru Wizara ya Màji Kwa jitihada kubwa zinazofanyika katika kuhakikisha changamoto za utoaji wa huduma ya maji zinapata majibu.
0 Comments
Post a Comment