DKT TULIA ACHANGIA MIFUKO 100 SARUJI SEKONDARI YA PANKUMBI.

Mbunge wa Mbeya Mjini na Naibu Spika wa Bunge JMT Dkt Tulia Ackson Januari 16, 2021 ametoa msaada wa saruji mifuko 100 kwa ajili ya shule ya sekondari Pankumbi iliyopo Kata ya Uyole Jijini Mbeya.

Pankumbi ni moja kati ya shule bora ambazo zinafanya vizuri kitaaluma ambapo mifuko hiyo itasaidia kufanya ukarabati wa madarasa wa shule hiyo.

Zaidi ya wanafunzi 1,500 waliotarajiwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza kwa mwaka 2021 wameshindwa kuingia madarasani hadi sasa kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.

Wadau mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson wamekuwa wakijitokeza kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kupunguza tatizo la wanafunzi kukosa vyumba vya kusomea kwa kidato cha kwanza.