USHUHUDA MZITO WA PROF MARK MWANDOSYA
‘’Kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja
nimekuwa nikiugua na kutibiwa ugonjwa wa #COVID19 unaotokana na virusi vya
CORONA(SARS-CoV-2).
Ni jinsi gani niliweza kuambukizwa
ugonjwa huu kijijini kwetu Lufilyo,Busokelo,Mbeya pamoja na kuzingatia tahadhari
zote dhidi ya maradhi haya Kitendawili.
Napenda Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa
zawadi ya uhai,zawadi ya Pasaka.Nawashukuru pia mke wangu Lucy Akiiki, watoto
na wajukuu, familia ya kahigwa na Mwandosya, Madaktari,Wauguzi wangu katika
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Hospitali Nairobi(Nairobi Hospital)
@AMREFFlyingdocs,Uongozi wa StanbicBankTz, Familia ya Balozi Chirau na mkewe Mama Rose Mwakwere wa
Nairobi Kenya, Familia ya Jaji wa Mahakama ya Juu nchini Uganda Mheshimiwa Paul na mkewe Mama Grace Mugamba na ndugu na marafiki
wote wanaoendelea kunitakia heri na afya njema, Asanteni sana.
Huu ni ushuhuda wangu kwamba
Corona/Covid19 ipo Tanzania, tumebahatika kupita kipindi hiki cha mpito salama
na kumpata Rais Mpya Mheshimiwa @SuluhuSamia,Mwenyezi Mungu amjaalie neema na Baraka
tele.
Nawaomba tena kwa unyenyekevu mkubwa Rais
Mheshimiwa Samia Suluhu,Makamu wa Rais Mheshimiwa Philipo Mpango na Mheshimiwa
Dkt Husein Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwamba
tuongozwe na Sayansi na Tuungane na tushirikiane na wenzetu duniani kote katika
kupambana na ugonjwa huu kama tunavyofanya katika milipuko ya magonjwa mengine
kwani katika mlipuko wowote hakuna anayeweza kuwa salama mpaka wote duniani
tumekuwa salama.
Maombi yangu kwa Mwenyezi Mungu ni
kwamba ikiwezekana Mtanzania awaye yote aepushwe na mateso na taabu za
kukabiliana na maradhi haya.
Hakika siwezi kumtakia mtu mwingine
yeyote, hata aliye adui yangu mkubwa namna gani kama yupo, apate ugonjwa huu.
Tutakiane Pasaka Njema,Mwenyezi Mungu
Ibariki Tanzania''.
0 Comments
Post a Comment