DKT TULIA AZIDI KUMALIZA UKATA WA VIJANA JIJINI MBEYA,
-Akabidhi Bodaboda na Bajaji za Sh Mil 62
Na Ripota wa
Mbeya Yetu
‘’Tulikuwa
tunakodishwa Bajaji kwa siku tunapeleka malengo kwa Bosi, siku nisipofikisha
malengo nahofia kunyang’anywa Bajaji anakabidhiwa dereva mwingine…sasa hivi hofu
hiyo itatoweka, namiliki Bajaji yangu mwenyewe mali yangu nitarejesha mkopo wangu
Tulia Trust’’.
Ndivyo
ambavyo amesikika kijana mmoja mwendesha Bajaji kutoka Jijini Mbeya
akidhihirisha furaha yake baada ya kukabidhiwa Bajaji kutoka Taasisi ya Tulia
Trust Januari 21,2021,zoezi ambalo limefanyika Stand ya Daladala Kabwe Jijini Mbeya likiwezeshwa na
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson.
Hizi ni
harakati za kuwakwamua vijana ili kuwezeshwa kujiajiri linalofanywa na Naibu
Spika Dkt Tulia Ackson ambaye pia ndiye Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini katika kuhakikisha vijana wengi ambao awali walikuwa ni
wazururaji wasio kuwa na kazi maalumu wanajiajiri.
Jumla ya
Bajaji 5 na Pikipiki 10 zenye thamani ya Tsh Mil 62 zimekopeshwa na Taasisi
ya Tulia Trust kwa Chama cha Bajaji na Bodaboda
Mbeya mjini kwa lengo la kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza
wakati wakati wa makabidhiano hayo katika kituo cha Daladala cha Kabwe Dkt
Tulia amesema kuwa Taasisi ya Tulia
Trust ipo kwa nia ya kuyawezesha makundi ya vijana kujikwamua kiuchumi.
‘’Leo hii
tunakabidhi Vijana Pikipiki 10 na Bajaji 5 zitakazosaidia kuwakwamua kiuchumi,
kuongeza uzalishaji ili kuendesha maisha yao ya kila siku’’amesema Dkt Tulia.
Dkt Tulia
amefafanua kuwa muendelezo huo wa mikopo umefuatia marejesho ya wakopaji wa
awali ambao wamerejesha mikopo yao kwa wakati na hivyo kusaidia wengine
kukopeshwa.
Amesema kuwa baadhi ya watu hudhani kuwa mikopo hiyo inapotolewa hadharani kuna baadhi ya makundi yamesahaulika bali amefafanua kuwa mikopo hiyo huwagusa watu aina zote wakiwemo wale wanaofika moja kwa moja ofisini yakiwemo makundi ya akina mama. .
Kadhalika
Dkt Tulia amezidi kusisitiza na kuwaomba wakazi wa Jiji la Mbeya kujiunga na
mfuko wa Bima ya Afya ili kuepuka gharama kubwa kwenye matibabu wakati
wanapougua.
AmesemaTaasisi ya Tulia Trust kwa kushirikiana na Ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya imeanzisha utaratibu wa kumuwezesha mwananchi mmoja mmoja kuchangia kiasi cha Tsh 30,000/- kwa mwaka ambayo inawekezekana kuchangia Tsh 100/- kila siku ambayo baada ya wiki moja hukabidhiwa kadi yake ya Bima ya Afya.
0 Comments
Post a Comment