Mbunge wa Jimbo la Lupa, wilayani Chunya mkoani Mbeya, chief Masache Njelu Kasaka, amefanya ziara katika mamlaka ya mji mdogo wa Makongolosi.

Pamoja na kusikiliza kero za wa wananchi na kuzitolea au kuzitafutia ufumbuzi, pia mh mbunge alikagua shughuli za biashara kwenye soko la Makongolos, ambako Mh mbunge amewaahidi wafanyabiashara hao mifuko 100 ya saruji  kwa ajili ya kumalizia sehemu ya soko iloyobakia.