Naibu Waziri wa Maji Mhandisi wa Maryprisca Mahundi amnyang'anya mradi wa maji Kinyangiri Singida Fasho Limited."Ashindwa kumaliza mradi kwa wakati"


 MkandarasiNaibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ameamuru kunyang'anywa mradi wa maji  wa Kijiji cha Kinyanyiri Wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida unaotekelezwa na Kampuni ya Fasho Limited ya Dodoma.

Mahundi amechukua hatua hiyo baada ya mkandarasi huyo kushindwa kukamilisha mradi huo unaogharimu milioni miatatu  ambapo amelipwa milioni mia moja themanini lakini umeshindwa kukamilika kwa zaidi ya miaka miwili sasa.


Mradi huo unaotarajiwa kuwanufaisha zaidi ya wananchi elfu nane wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari umekuwa ni kikwazo kutokana na wananchi kulazika kutumia maji ya mtoni ambayo si salama kwa afya jambo lililomkera Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi.


Akitotoa taarifa ya mradi huo mbele ya Naibu Waziri Mhandisi wa Maji Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini(RUWASA) Wilaya ya Mkalama Andidus Muchunguzi alisema licha ya Mkandarasi kulipwa pesa za serikali lakini ameshindwa kuumaliza kwa wakati sambamba na kupuuza agizo la Naibu Waziri lillilomtaka kuwepo eneo la mradi.


Meneja wa RUWASA Mkoa wa Singida Mhandisi Lucas Said alisema mradi huo umehusisha ujenzi wa tanki la maji,nyumba ya mashine ya kuvuta maji,usambazaji wa mabomba ya maji na vituo vya kuchotea maji(Vioski).


Baada ya kupokea taarifa ya Meneja wa RUWASA Wilaya na Mkoa Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi aliagiza Wakandarasi wote nchini ambao wameshindwa kuikamilisha miradi kwa wakati wanyang'anye na kukabidhiwa RUWASA ili waitekeleze pia Wakandasi hao wasipewe miradi mingine.


Alisema Rais ametoa pesa nyingi za miradi mbalimbali ya maji nchini hivyo haoni sababu za miradi kushindwa kukamilika kwa wakati.


Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Singida alisema Lucas Said alisema baada ya kukabidhiwa mradi huo aliahidi kuukamilisha katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja ili kuwaondolea adha wananchi zaidi ya elfu nane.


Miradi mingi nchini imeshindwa kukamilika kwa wakati kutokana na baadhi ya Wakandarasi kutokuwa waaminifu pia watumishi wa RUWASA kutoitembelea miradi hivyo serikali kushindwa kufikia malengo yake.


Katika kampeni yake Rais John Pombe Magufuli aliahidi kuondoa kero ya upatikanaji wa maji nchini.