MAMA SAMIA AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI MBUNGE KASAKA AUNGANA NA WACHIMBAJI CHUNYA .
Makamu wa
Rais Mama Samia Suluhu Hassan amefungua Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji
sekta ya Madini katika Ukumbi wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam Kongamano
ambalo pia limehudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Lupa Wilayani Chunya Mhe.Masache
Njelu Kasaka.
Mheshimiwa
Masache ameungana na Wachimbaji wa Madini kutoka Wilayani Chunya Mkoani Mbeya Wilaya
abayo ni moja katika wilaya mashuhuri kwa uchimbaji wa dhahabu hapa nchini.
Akizungumza
katika Kongamano hilo Makamu wa Rais Mama Samia amesema serikali ina nia ya
kusaidia wachimbaji wadogo kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya
madini kwa wachimbaji wadogo na wakubwa na kuwa serikali inanufaika kutokana na
kodi zinazolipwa na wawekezaji katika sekta ya madini.
0 Comments
Post a Comment