Kwaheri Bosi!! Ndivyo inavyoonekana viongozi hawa wa Serikali Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri Dkt Tulia Ackson na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi walipokuwa wakiuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi Wilayani Korogwe Mkoani Tanga.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dkt Tulia Ackson akitoa salamu za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi nyumba kwa marehemu Korogwe mkoani Tanga.


Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akiweka saini kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi nyumbani Korogwe Mkoani Tanga.
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi nyumbani kwake Korogwe Mkoani Tanga.