MBUNGE MH SUMA FYANDOMO AWATIA MOYO WANAWAKE WA MKOA WA MBEYA
Mbunge Viti
Maalum Mkoa wa Mbeya Suma Fyandomo amewatia moyo akina mama na kuwataka
kujitokeza katika shughuli zote wanazodhani kuwa zinafanywa na wanaume pekee.
Fyandomo
amesema kuwa Mwanamke ndio nguzo ya familia na anatakiwa ajitambue kuwa yeye
ndiye nguzo ya familia kwa kuwa jambo lolote linaloihusu familia mwanamke ndiye
anakuwa mtu wa kwanza kutolea majibu.
Amesema
wakati wa kuwasubiri wanaume kutekeleza majukumu ya kifamilia zimepitwa na
wakati ni vyema akina mama kusimama kidete katika kusimamia familia ili kusaidia
sehemu ya majukumu ya wanaume.
Mbunge Suma
Fyandomo amesisitiza kuwa majukumu yote yanayofanywa na mwanaume katika kusimamia
na kuitunza familia yanaweza kufanywa na mwanamke hivyo ni vyema wanaume
wakapunguziwa mzigo ili sehemu inayobaki itekelezwe na mwanamke.
Fyandomo ni
mmoja kati ya Wabunge watatu viti maalumu wanaowakilisha mkoa wa Mbeya akiwemo
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi na Bahati Ndingo
anayewakilisha wazazi Taifa.
0 Comments
Post a Comment