Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ameendeelea kutoa Wito na Maagizo kwa Watendaji na Mameneja wa Wakala wa Maji RUWASA walioteuliwa hivi karibu kuhakikisha wanakwenda kufanya kazi kwa ushirikiano.

                                                 
Mhandisi Maryprisca pia amewataka kuhakikisha wanawajibika ipasavyo huku wakisimamia kauli mbiu ya RUWASA ya Maji Bombani na wananchi wahakikishiwe wanapata maji ya uhakika kwa wakati.

‘’Mkatoe Ushirikiano kwa Viongozi wa maeneo mnayokwenda kufanya kazi’’Amesema Mhandisi Maryprisca Mahundi.