TUNAENDELEA KUKULILIA BABA!!

‘’Tunaendelea kumlilia Mpendwa Wetu,Jemedari Hayati Dkt John Pombe Magufuli aliyetuaga March 17, sisi kama vijana wake tutaendelea kumuenzi kwa kuchapa kazi kama alivyotufundisha kamwe haturudi nyuma.

Nguvu ile ile aliyotuachia Mzee wetu Hayati Dkt Magufuli tutaiendeleza kwa Mama yetu Kipenzi Rais Samia Suluhu Hassan, kamwe hatutamuangusha’’ amesema Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi alipokuwa akitia saini kitabu cha maombolezo cha Hayati Dkt John Pombe Magufuli Bungeni Jijini Dodoma leo.

Watanzania wapo katika maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Magufuli ambapo mrithi wake Rais Mama Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 21 za maombolezo huku bendera zikipeperushwa nusu mlingoti.

Hayati Dkt Magufuli amezikwa March 26 nyumbani kwake Chato Mkoani Geita ambapo maelfu ya watu walihudhuria mazishi yake huku mamilioni ya Watanzania wakishuhudia mazishi hayo kupitia runinga.