Suma Fyandomo Katika Kamati ya Bunge Sheria na Katiba

Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Suma Fyandomo amekuwa ni kati ya wabunge waliopo kwenye Kamati ya Bunge, Sheria na Katiba kutembelea Mahakama mbalimbali mikoa ya Dodoma, Morogoro na Njombe.

Ziara hiyo iliambatana na  ukaguzi wa ujenzi wa mahakama na  tathmini yake kwa fedha za ujenzi wa mahakama hizo.

March 12 Kamati ilifanya ukaguzi Mahakama ya Kibaigwa mkoani Dodoma,March 13 kamati ilifika mkoani Njombe na kufanya ukaguzi ambapo March 14 kamati ilikagua maendeleo ya ujenzi mahakama ya mkoa wa Morogoro.

Katika ziara hiyo Waziri wa Katiba na Sheria na Mwigulu Nchemba ameambatana pia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt Adelardus Kilangi.