MAZIKO YA ASKOFU MWENISONGOLE MHANDISI MARYPRISCA ATOA NENO LA FARAJA KWA MBUNGE WA MBOZI
Na Mwandishi Wetu, Mbozi
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ameshiriki ibada ya mazishi ya Baba mzazi wa Mbunge wa jimbo
la Mbozi George Mwenisongole,Askofu wa tatu wa Kanisa la TAG Ranwell
Mwenisongole.
Ibada hiyo ambayo
imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wa vyama vya siasa imefanyika
katika Uwanja wa CCM Vwawa Mbozi Mkoa wa Songwe.
Akitoa salamu za pole
Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye ni Mbunge wa Vitimaalumu Mkoa wa Mbeya
amemtaka Mbunge wa Mbozi, Mwenisongole kuwa na subira katika kipindi hiki cha
majonzi ya kuondokewa na mzazi.
Kadhalika Mhandisi Mahundi ametoa pole kwa waumini wa Kanisa la TAG akiwasihi waendelee kushikamana na kufuata nyayo za Askofu Ranwell Mwenisongole wakiendelea kumtumikia Mungu bila kutofautiana.
Ibada ya maziko ya
Askofu Mwenisongole ilifuatia na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu
eneo la Ichenjezya Wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe.
0 Comments
Post a Comment