MHANDISI MARYPSRISCA ACHANGIA SHILINGI LAKI SITA KUSAPOTI WENYE MAHITAJI MBALIZI

    Na Mwandishi wa MbeyaYetu   

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amechangia jumla ya shilingi laki  sita na nguo kwa ajili ya kuwahudumia wenye mahitaji katika kituo cha Iwindi na Hospitali Teule ya Ifisi wilaya ya Mbeya. 

Mhandisi Maryprisca ambaye pia ni Mbunge wa Viti maalumu anayewakilisha mkoa wa Mbeya amechangia fedha hizo kwenye tamasha maalumu lililoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya Dorcas Twaweza wakati wa mkesha wa mwaka mpya uliofanyika Mamlaka  ya mji mdogo wa Mbalizi. 

Kikundi hicho kimekusanya jumla ya shilingi laki tano ikiwa ni mchango  wa awali ambapo kikundi hicho kinatarajia kuwatembelea wenye mahitaji Januari 2, 2022. 

Jumla ya shilingi milioni moja laki mbili elfu hamsini na moja mia nne zimekusanywa kwa ajili ya kuwatembelea na kuwasaidia wenye  mahitaji. 

Mhandisi Maryprisca  amewapongeza wadau na baadhi ya wananchi wa Mamlaka ya mji mdogo wa  Mbalizi kutokana na mshikamano wao waliouonesha hasa wakilenga kuwatembelea na kuwaona wenye mahitaji.