Eng. Maryprisca aunga mkono ujenzi wa nyumba Katibu UWT Chunya, Mil 12 zachangwa



 

Na Mwandishi Wetu Chunya.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya na Diwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka wanawake wa Wilaya ya Chunya kujifunza kwa wengine wamudu kumiliki  uchumi wao bila kuwategemea wanaume.

Mhandisi Maryprisca ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji ameyasema hayo katika sherehe ya usiku wa mwanamke iliyofanyika Chunya Mjini kwa lengo la kujifunza ujasiriamali,afya na kuchangia ujenzi wa nyumba kwa ajili ya Katibu wa Umoja wa Wanawake(UWT)Wilaya ya Chunya.

Amesema iwapo wanawake watafanikiwa kumiliki uchumi wao watamudu kuwasaidia wanaume kusomesha watoto pia hata kumiliki nyumba bora za kisasa.

Amehimiza wanawake kwenda mikoa mingine kujifunza na kubadilishana uzoefu badala ya kubweteka mahala pamoja na kufanya shughuli zisizo na tija.

Mahundi ameahidi kuchangia shilingi milioni mbili ambapo wadau wengine wamechangia jumla ya shilingi milioni kumi na saba ikiwa ni fedha taslim shilingi milioni tatu.pamoja na vifaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya saruji huku  Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akiahidi kuungaa mkono ujenzi huo kwa kuchangia mifuko ya saruji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa sherehe Anjela Sompo mbali ya kumshukuru Naibu Waziri wa Maji kuitikia wito ambapo pia wametumia fursa ya usiku huo  kujifunza ujasiriamali na upendo kwa wanawake na afya ya uzazi.