Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii NSSF mkoa wa Mbeya umemaliza wiki ya huduma kwa wateja kwa mafanikio huku tishio la kuwaburuza mahakamani Waajiri wasiochangia wafanyakazi wao wakisalimu amri.
Meneja NSSF Mkoa wa Mbeya Deus Jandwa amesema taarifa zilizotolewa za uwaburuza mahakamani Waajiri wasiochangia mfuko wa hifadhi zimezaa matunda.
Amesema waajiri wamejitokeza na kukaa mezani kujadili njia zitakazossidia kutowakwamisha wafanyakazi na Wastaafu.
Jandwa amesema lengo la Mfuko wa hifadhi si kwa ajili ya kuwakomoa waajiri bali kuhakikisha wanachama wanapata haki zao kwa wakati kulingana na makubaliano.
"Wamekuja tumekaa nao na kuwapa utaratibu mzuri wa kuchangia wafanyakazi wao oasipo kuathiri shughuli zao"
Amewataka wanachama kuwa karibu na NSSF ili kutumia mifumo ya kidigitali kupitia simu janja na kuendelea kupata taarifa kulingana na mapato ambayo ni asilimia 20 ya mapato ya mwezi.
Wiki ya huduma kwa wateja duniani iliyoanza Oktoba 3 imemalizika Oktoba 7 huku NSSF ikiwa na kauli mbiu yake ya Huduma Bora Kipaumbele chetu.

0 Comments
Post a Comment