Rose Mwalongo Mshauri kutoka Mtandao wa Kijinsia(TGNP)anaeleza lengo la kuandaa mafunzo hayo yatayodumu kwa siku tano Mkoani Mbeya ni kuwapitisha washiriki katika kuchanganua bajeti za halmamashauri kama zinazingatia masuala ya afya,maji,elimu,mazingira na tabia nchi.

Katika mafunzo hayo washiriki wataungana na watendaji wa halmashauri ya Mbeya ili kubalishana uzoefu namna halmashauri hiyo inavyopanga bajeti zake kuzingatia mahitaji muhimu.

Shirika lisilo la Kiserikali la Mtandao wa Kijinsia nchini(TGNP)linawajengea uwezo viongozi mbalimbali wa vituo vya taarifa na maarifa Mkoani Mbeya kwa lengo la kupitia bajeti za halmashauri endapo zinazingatia mlengo wa kijinsia.

 Rose Mwalongo Mshauri kutoka Mtandao wa Kijinsia(TGNP)anaeleza lengo la kuandaa mafunzo hayo yatayodumu kwa siku tano Mkoani Mbeya ni kuwapitisha washiriki katika kuchanganua bajeti za halmamashauri kama zinazingatia masuala ya afya,maji,elimu,mazingira na tabia nchi.

 Katika mafunzo hayo washiriki wataungana na watendaji wa halmashauri ya Mbeya ili kubalishana uzoefu namna halmashauri hiyo inavyopanga bajeti zake kuzingatia mahitaji muhimu.

 Katibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Juhudi Mwajunga kutoka Kata ya Igale Halmashauri ya Mbeya amesema mwitikio kwa halmashauri umekuwa ni mkubwa kwani halmashauri ya Mbeya imekuwa ikitenga bajeti ya vyumba vya kujisitiri na taulo za kike.

 Pamoja na juhudi zinazofanywa kwa ushirikiano mkubwa baina ya vituo vya taarifa na maarifa wananchi wamekuwa wakijiamini hata kuchangia mawazo yao kwenye vikao mbalimbali.

 Aidha Mariam Mgawe kutoka kituo cha Tigushe Kata ya Ijombe amesema kutengwa kwa bajeti ya taulo za kike umeongeza mahudhurio ya watoto wa kike madarasani tofauti na awali ambapo watoto wanapokuwa hedhi hushindwa kuhudhuria masomo kwa zaidi ya siku tano hali inayowafanya kuzorota katika masomo.

 Hata hivyo wanawake wamekuwa wakiunganisha nguvu zao hata kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake ambapo kwa sasa vitendo hivyo vimepungua kutokana na kufichuliwa na baadhi ya wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

 Tangu kuanzishwa kwa TGNP kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye jamii ikiwa ni pamoja na ongezeko kubwa idadi ya wanawake kwenye nafasi za uongozi.