Picha ya pamoja kati ya Meneja wa TCRA Ofisi ya Zanzibar Bi. Esuvatie Masinga(aliejifunga mtandio mweupe), Maafisa wa TCRA na Wakuu wa Skuli za Sekondari Zanzibar muda mfupi baada ya kuhitimishwa Mkutano wa Jumuiya ya Walimu Wakuu wa Skuli za Sekondari Zanzibar (JUWASEZA) uliofanyika kisiwa cha Pemba kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni. Katika Mkutano huo TCRA ilitoa elimu kuhusu uanzishwaji wa Klabu za Kidijiti katika Skuli za Sekondari Zanzibar. Picha na TCRA.
Meneja wa TCRA Ofisi ya Zanzibar Bi. Esuvatie Masinga akitoa elimu kuhusu uanzishwaji wa Klabu za Kidijiti katika Skuli za Sekondari Zanzibar wakati akizungumza na Wakuu wa Shule kwenye Mkutano wa Jumuiya ya Walimu Wakuu wa Skuli za Sekondari Zanzibar (JUWASEZA) uliofanyika kisiwa cha Pemba kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni. Picha na TCRA.


Na Mwandishi Wetu – Pemba

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ofisi ya Zanzibar imetoa elimu kuhusu Uanzishwaji na Uendeshaji wa Klabu za Kidijiti kwa Wakuu wa Skuli za Sekondari Zanzibar (JUWASEZA) kwenyekikao-kazi kilichofanyikaJumatano hii, Pemba.

 Meneja wa Mamlaka hiyo Ofisi ya Zanzibar, Bi. Esuvatie Masingaakizungumza mara baada ya seminahiyo alisema Wakuu wa Skuli za Sekondari ni msingi muhimu katika kuhakikisha Klabu za Kidijiti zinaanzishwa kwenye skuli na kuendeshwailiziwanufaishe wanafunzi kuwa washirikikamili katika kujenga uchumi wa kidijiti na buluu.

 “Ushiriki wa vijana kwenye uchumi wa kidijiti na buluu ni wa msingi sana; hii ndiyosababutumeazimiakuwafikia wanafunzi kupitia wakuu wa skuli kwa kuwa wanayonguvu ya ushawishi kama Viongozi watakaochagiza Uanzishaji wa klabu hizi muhimu,” alisema.

 Masinga alibainisha kuwa ilikujenga uchumi wa kisasaunaoegemea zaidi matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano, ushiriki wa vijana ni muhimu sana.

 “Vijana ndiyonguzo muhimu ya kuimarisha na kujenga uchumi wa kidijiti, lengoletu ni kuhakikisha vijana wanajiunga na kuwa washiriki wa Klabu za Kidijiti zitakazowapatiamaarifa ya teknolojia kupitia masomo ya STEM yaaniHisabati, Sayansi, Teknolojia na Uhandisi,”

 Alisema TCRA itaendelea kuhamasisha ubunifu na uvumbuzi katika klabu za kidijiti zilizoanzishwa na zitakazoanzishwa ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo waratibu wa klabu za kidijiti ili waweze kuzisimamia vyema ziweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.

 “TCRA tunaamini Wakuu wa Skulimtasaidiauanzishwaji wa klabu za kidijiti katika skulizenu. Ikumbukwe kuwa klabu hizi hazinatofauti na klabu nyingine za masomo kama klabu za Hisabati, Kiingerezanakadhalika. Ili tujenge uchumi wa kidijiti na buluu matumizi ya TEHAMA hayaepukikihivyo ni tunapaswatuwaandae vijana wetu”alisema Masinga.

 Aliwaasa wanafunzi pamoja na walimuambao ni walezikujiunga kwenye klabu za kidijiti kwa kujisajilimoja kwa moja kupitia tovuti ya https://digitalclubs.tz au kuzianzishamoja kwa moja katika skulizao kwa kupata utaratibu wa uanzishaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa JUWASEZA Khatibu Rashidi aliishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Ofisi ya Zanzibar kwa kuona umuhimu wa kuwapawalimuwakuu Elimu ya Uanzishaji wa Klabu za Kidijiti akisemazitakuwazenye mchango mkubwa katika kuwahamasisha wanafunzi kuifahamu zaidi Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

 “Hakikatumefaidi sana kwa seminaambayommetupatia, huu ni msingimzuri wa kuwajengea uwezo wanafunzi wetu hasa tutakapoanzishaklabuhizi kwenye skulizetu,” alisisitiza.

 Mkutano huo wa 11 wa JUWASEZA ulifunguliwa na Waziri wa Elimu ya Mafunzo ya Amali Mheshimiwa Lela Muhammed Mussaambaealiwasisitizawalimukutekelezamajukumuyao ipasavyo.