NAIBU Waziri wa Maji Mhe.Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amemuagiza Meneja wa Ruwasa wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Mhandisi Erwin Sizinga aweze kuhakikisha wanakamilisha ulazaji wa bomba wa umbali wa kilomita 2.8 ndani ya wiki moja ili wananchi wa Kata ya Ubiri na Ngulwi waweze kupata huduma ya maji safi na salama.
Kadhalika Mhandisi Mahundi amemuagiza Mkandarasi anayejenga Mradi wa Maji wa Magamba ahakikishe anaongeza kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ili aweze kukamilisha kwa wakati.
Mhandisi Mahundi ametoa maagizo hayo leo Januari 6 2024, alipotembelea na kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji ya Magamba na Mradi ya Maji Irente-Yoghoi-Ngulwi iliyopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

 *MAHUNDI ATOA SIKU SABA MENEJA RUWASA LUSHOTO KUKAMILISHA ULAZAJI WA MABOMBA* .

NAIBU Waziri wa Maji  Mhe.Mhandisi Maryprisca  Mahundi (Mb) amemuagiza Meneja wa Ruwasa wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Mhandisi Erwin Sizinga aweze kuhakikisha wanakamilisha ulazaji wa bomba wa umbali wa kilomita 2.8 ndani ya wiki moja ili wananchi wa Kata ya  Ubiri na Ngulwi waweze kupata huduma ya maji safi na salama.

Kadhalika  Mhandisi Mahundi amemuagiza Mkandarasi anayejenga Mradi wa Maji wa Magamba ahakikishe anaongeza kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ili aweze kukamilisha kwa wakati.

Mhandisi Mahundi ametoa maagizo hayo leo Januari 6  2024, alipotembelea na kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji ya Magamba na Mradi ya Maji Irente-Yoghoi-Ngulwi iliyopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

"Ili wananchi  elfu 30,835 wa maeneo ya Magamba, Kwesimu, Bara, Jegestal, Kambi namba nne, Chakechake, Kitivo, Maguzoni, Sinza, Lushoto Mjini, Mabwawani, Kipembe na Kialilo waweze kupata huduma ya maji miradi hii inapaswa kukamilika kwa wakati"amesema Mhandisi Mahundi 

Naye  Mbunge wa Jimbo la Lushoto, Mhe. Shaban Shekilindi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutekeleza miradi ya maji kwenye jimbo hilo huku akisema  wananchi wengi watapata huduma ya maji huku akiwasisitiza wakandarasi kukamilisha kwa wakati.

Mwisho