NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemuagiza  Mkandarasi anayetekeleza Miradi ya Maji ya Funta na Mradi wa Maji wa Wanga  iliyopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga kuwa miradi hiyo iweze kukamilika kabla ya  Aprili 30, 2024  huku akisema itakapofika  muda huo hatapewa muda wa nyongeza.
 
Kukamilika kwa miradi hiyo  kunatarajia kunufaisha  wananchi   elfu 7121 wa Wilaya  ya Lushoto  katika kupata huduma ya maji safi na salama.
Mhandisi  Mahundi ametoa agizo hilo  leo Januari 8  2024  alipotembelea na kukagua utekelezaji wa miradi hiyo miwili  kwenye Jimbo la uchaguzi Bumbuli lililopo Wilayani Lushoto 
"Utekelezaji wa  Mradi wa Maji Funta ulianza rasmi Agosti 18 2022 na ulipaswa kukamilika ndani ya siku 270  lakini mpaka sasa haujakamilika naomba nisisitize itakapofika April  30 hakutakuwa na kuda wa nyongeza tunahitaji wananchi  4782 wa maeneo ya Funta na Manga, na  wananchi   wa kijiji cha  Manga na Kwemkole  2339 waweze kupata huduma" amesema Mhandisi Mahundi

Naye  Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mheshimiwa  Kalist Lazaro ameahidi kumsimia kwa karibu Mkandarasi huyo ili  miradi hiyo itekelezwe  kwa wakati na wananchi waweze kupata huduma ya maji 

MHANDISI MAHUNDI AMKALIA KOONI MKANDARASI MIRADI YA MAJI FUNTA NA WANGA LUSHOTO 

📌ASEMA HATAPEWA MUDA WA NYONGEZA 

📌WANANCHI 7121 KUNUFAIKA NA MAJI BAADA YA KUKAMILIKA 

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemuagiza  Mkandarasi anayetekeleza Miradi ya Maji ya Funta na Mradi wa Maji wa Wanga  iliyopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga kuwa miradi hiyo iweze kukamilika kabla ya  Aprili 30, 2024  huku akisema itakapofika  muda huo hatapewa muda wa nyongeza.

Kukamilika kwa miradi hiyo  kunatarajia kunufaisha  wananchi   elfu 7121 wa Wilaya  ya Lushoto  katika kupata huduma ya maji safi na salama.

Mhandisi  Mahundi ametoa agizo hilo  leo Januari 8  2024  alipotembelea na kukagua utekelezaji wa miradi hiyo miwili  kwenye Jimbo la uchaguzi Bumbuli lililopo Wilayani Lushoto 

"Utekelezaji wa  Mradi wa Maji Funta ulianza rasmi Agosti 18 2022 na ulipaswa kukamilika ndani ya siku 270  lakini mpaka sasa haujakamilika naomba nisisitize itakapofika April  30 hakutakuwa na kuda wa nyongeza tunahitaji wananchi  4782 wa maeneo ya Funta na Manga, na  wananchi   wa kijiji cha  Manga na Kwemkole  2339 waweze kupata huduma" amesema Mhandisi Mahundi

Sambamba na hayo Mhandisi Mahundi amewataka wananchi kuendelee kutunza miundombinu ya maji pamoja na vyanzo vyake ili miradi inayotekelezwa iwe endelevu.

Naye  Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mheshimiwa  Kalist Lazaro ameahidi kumsimia kwa karibu Mkandarasi huyo ili  miradi hiyo itekelezwe  kwa wakati na wananchi waweze kupata huduma ya maji 

Hata hivyo ikumbukwe kuwa Mradi huo unagharimu jumla ya Shilingi za Kitanzania Milioni 832.6 na baada ya kukamilika unaenda kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama  kwa wananchi. 

Mwisho