Ujenzi wa barabara ya Lupeta-Wimba -Izumbwe yenye urefu wa Km.9.5 na ile ya Inyala-Simambwe Km. 16.7 kwa kiwango cha lami imelenga kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi mkoani Mbeya kwa kurahisisha usafirishaji wa mazao kwa urahisi.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Dennis Londo wakati wa ziara  ya kukagua miradi ya elimu na miundombinu ya Barbara mkoani  Mbeya.

Mhe. Lundo alisema kuwa kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja chini ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

Wakati huo huo Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa TARURA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Barabara Mhandisi Venant Komba alisema kuwa katika Mkoa wa Mbeya TARURA inaendelea na utekelezaji wa  miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya barabara zinazofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya chini ya mradi wa Agri Conect. 
Naye, Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila alisema wamepokea maelekezo yote yaliyotolewa na kamati hiyo na kuahidi kufanyia kazi mapendekezo yote.

Ujenzi barabara ya Lupeta-Wimba-Izumbwe kuinua Uchumi wa wananchi Mbeya.

Mbeya

Ujenzi wa barabara ya Lupeta-Wimba -Izumbwe yenye urefu wa Km.9.5 na ile ya Inyala-Simambwe Km. 16.7 kwa kiwango cha lami imelenga kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi mkoani Mbeya kwa kurahisisha usafirishaji wa mazao kwa urahisi.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Dennis Londo wakati wa ziara  ya kukagua miradi ya elimu na miundombinu ya Barbara mkoani  Mbeya.

Mhe. Lundo alisema kuwa kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja chini ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

"Kazi kubwa na yenye viwango imefanyika katika elimu na miundombinu katika Halmashauri hii, Miradi hii miwili ya barabara tuliyotembelea ni muhimu  kwa uchumi wa Mbeya lakini na Taifa kwa ujumla”Alisema Mhe. Londo

Kwa upande wa uchumi Mhe. Londo alisema barabara hizo zitaeda kurahisisha shughuli za kilimo na kupunguza  gharama za pembejeo na uzalishaji kwani  gharama za usafirishaji  zitapungua, hivyo kumuongezea kipato mkulima mmoja mmoja na kumuondolea umaskini mwananchi.

Naye, Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila alisema wamepokea maelekezo yote yaliyotolewa na kamati hiyo na kuahidi kufanyia kazi mapendekezo yote.

Wakati huo huo Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa TARURA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Barabara Mhandisi Venant Komba alisema kuwa katika Mkoa wa Mbeya TARURA inaendelea na utekelezaji wa  miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya barabara zinazofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya chini ya mradi wa Agri Conect. 

Mhandisi Komba alisema kuwa kwa  barabara ya Lupeta-Wimba ipo katika hatua za mwisho na itakamilika katikati ya mwezi Februari, mwaka huu.

Agri Connect ni mpango unaotekelezwa na TARURA kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) na madhumuni ya ujenzi  ni kukuza uchumi wa Mkoa pamoja na nchi kwa ujumla, kuchochea maendeleo ya sekta binafsi, kutengeneza ajira kwenye sekta ya kilimo na kuongeza thamani ya mazao ya biashara yaliyopo ndani ya Mkoa.

MWISHO