Wataalamu wa afya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wametakiwa kutoa huduma za afya kwa upendo na kuzingatia utu wawapo katika maeneo yao ya kazi.     

Hayo yamesemwa leo tarehe 21 Februari, 2024 na Dkt. Godlove Mbwanji, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo zaidi wahudumu wa afya watarajali katika eneo la utaoji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaoishi na virusi ya UKIMWI.
kwa hiyo wahudumieni wagonjwa vizuri, waonyeshe upendo, kwa kuwa upendo una nguvu kuliko hata dawa tunazo wahudumia”. – Dkt. Godlove Mbwanji

WATOA HUDUMA ZA AFYA WAHIMIZWA KUHUDUMIA WAGONJWA KWA UPENDO NA  KUZINGATIA UTU

Wataalamu wa afya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wametakiwa  kutoa huduma za afya kwa upendo na kuzingatia utu wawapo katika maeneo yao ya kazi.     

Hayo yamesemwa leo tarehe 21 Februari, 2024 na Dkt. Godlove Mbwanji, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo zaidi wahudumu wa afya watarajali katika eneo la utaoji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaoishi na virusi  ya UKIMWI.

“..kwa hiyo wahudumieni wagonjwa vizuri, waonyeshe upendo, kwa kuwa  upendo una nguvu kuliko hata dawa tunazo wahudumia”. – Dkt. Godlove Mbwanji

Nae Michael Mwagala ambaye ni maratibu wa mafunzo hayo amesema mafunzo hayo ya siku tatu yamehusisha watoa huduma za afya watarajali wakiwemo, Madaktari, Wauguzi pamoja na watalaamu wa maabara na kuendeshwa na wakufunzi kutoka Idara mbalimbali hospitalini hapo.

“.. mafunzo haya yanahusisha wawezeshaji kutoka idara mbalimbali hospitalini hapa kwaajili ya kuwajengea watarajali hawa uwezo zaidi wa kuwahudumia wagonjwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI”. – Michael Mwagala 

George Andrew ambaye ni kiongozi wa watoa huduma za afya watarajali hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ameushukuru Uongozi wa hospitali na kusema mafunzo hayo yatakayofanyika kwa muda wa siku tatu yatakuwa msaada katika utendaji wao utaoji huduma za matibabu kwa wagonjwa hao wanaoishi na virusi vya UKIMWI.

“..naami tumepokea mengi ambayo yamezungumzwa na yatatusaidi katika utendaji wetu hivyo tutafanya kazi kwa bidii na kwa uaminifu kwa kuyazingatia yale tuliyoambiwa”. – George Andrew