KAMPUNI YA MAJINJAH YAANZISHA KIWANDA CHA KAHAWA ''MAJINJAH COFEE
CURRING''
Na Ripota wa Mbeya Yetu,Mbozi.
Katika kuunga mkono Serikali ya awamu ya Tano kuelekea Nchi ya Viwanda Kampuni ya Majinjah Logistics Limited inayojishughulisha zaidi na Usafirishaji wa Mabasi ya Abiria na Mizigo imeamua kuelekeza nguvu zake katika uwekezaji wa Viwanda na Kilimo.
Majinjah
Logistics Company Limited ni kampuni yenye makampuni mengi baadhi yake
yakiwemo kampuni ya usindikaji wa Maji safi ya Kunywa ya Tukuyu
Springs Water iliyopo Kibisi Wilayani Rungwe,Kiwanda cha Usindikaji wa Sembe cha
Majinjah Mill kilichopo Kibaha Picha ya Ndege mkoani Pwani na Mabasi ya Usafirishaji
wa abiria na mizigo kupitia Majinjah Special mikoa mbalimbali nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah Logistics Limited Alinanuswe Ahobhokile Kabungo
‘’Mzee Majinjah’’ anaeleza Majinjah Logistics imeanza kujikita kwenye shughuli
za Kilimo na uwekezaji wa Viwanda, kwa sasa imeanza katika uwekezaji kwenye
uanzishwaji wa kiwanda cha Kusindika Kahawa katika Kijiji cha Igamba wilayani
Mbozi Mkoani Songwe.
Mzee
Majinjah anasema sera ya Uwekezaji ambayo ni maoni ya Rais Dkt John Magufuli
imehamasisha wawekezaji kujitokeza kwa wingi katika maeneo ya uwekezaji wa
Viwanda na kuwa Majinjah imeamua kujenga kiwanda cha Kahawa karibu kabisa na
wakulima maeneo ya vijijini.
Anafafanua
kuwa uwekezaji katika mkoa mpya wa Songwe utazidi kuufanya mkoa huo kushindana
na hata kuipiku mikoa ya zamani kutokana na mkoa huo kuwa kinara katika
uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara.
Anasema Wakulima
wa Zao la Kahawa Wilayani Mbozi wataanza kunufaika kwa uwepo wa kiwanda hicho
karibu na maeneo yao na kuwa awali kahawa ilikuwa ikisafirishwa kwa ajili ya
ukoboaji Jijini Mbeya.
Kuhusu
kuwasaidia wakulima wazalishe Kahawa bora Mzee
Majinjah amesema watashirikiana na wakulima katika kutoa elimu ya Kilimo bora
na kwa kupitia kikundi cha Wakulima wa Kahawa Mawanga AMCOS wataketi na
kuhamasishana kilimo bora chenye tija.
Katika
kuhakikisha wakulima wa zao la kahawa wilayani Mbozi wanaepuka kupunjwa kwa kuuza
mazao yao yakiwa shambani KATA KICHWA wanachama wa MAWANGA AMCOS wamehamasishwa kutouza kahawa yao mapema
kuepuka kudhulumiwa wakati wa mavuno.
0 Comments
Post a Comment