MAMA SAMIA AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI   MBUNGE KASAKA AUNGANA NA WACHIMBAJI CHUNYA .


Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan amefungua Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji sekta ya Madini katika Ukumbi wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam Kongamano ambalo pia limehudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Lupa Wilayani Chunya Mhe.Masache Njelu Kasaka.

Mheshimiwa Masache ameungana na Wachimbaji wa Madini kutoka Wilayani Chunya Mkoani Mbeya Wilaya abayo ni moja katika wilaya mashuhuri kwa uchimbaji wa dhahabu hapa nchini.

Akizungumza katika Kongamano hilo Makamu wa Rais Mama Samia amesema serikali ina nia ya kusaidia wachimbaji wadogo kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya madini kwa wachimbaji wadogo na wakubwa na kuwa serikali inanufaika kutokana na kodi zinazolipwa na wawekezaji katika sekta ya madini.

Kwa upande wake Mbunge wa Lupa Mh.Masache Njelu Kasaka amesema Kongamano hilo mbali ya kuwakutanisha wachimbaji wa Kimataifa na wachimbaji wa hapa  nchini linafungua fursa kwa wachimbaji wadogo hususan kwa wachimbaji wazawa na kuambukizwa uzoefu kutoka Makampuni makubwa ya Uchimbaji Madini.