MARYPRISCA:’’SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZOTE ZA MAJI MKOANI GEITA’’                                                   


                                Na Ripota wa Mbeya Yetu,Geita

Ni mwendelezo wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi kanda ya Ziwa, mara hii akiwa Mkoani Geita ambako amekagua utekelezaji wa miradi ya Maji mkoani humo. 

Ndani ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Maryprisca Mahundi amepokea taarifa zinazohusu changamoto za upatikanaji wa maji katika miji ya Katoro,Mbongwe na Bukombe kutoka kwa Mkuu wa mkoa huo Robert Gabriel. 

Akizungumza Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameahidi kutatua changamoto zote za maji mkoani humo na kuwataka watendaji wa RUWASA kushirikiana ili kuunga mkono jithada za serikali hususani katika Kauli Mbiu ya RUWASA ya Maji Bombani sanjari na kumtua Mama ndoo kichwani.